NGULI WA SIASA NCHINI ALIYESHIKA UDIWANI TOKA 1988 HADI SASA AELEZA ALIVYOIPAMBANIA KATA YA BARA.
MAKALA
-aeleza mafanikio ikiwemo kujenga shule za msingi kila kijiji wastafu Rais Kikwete na waziri mkuu Sumaye.
‘’miaka 10 iliyopita wagonjwa wa kata hiyo yenye wakazi 30,000 wakiwemo wajawazito walitibiwa kwa waganga wa tiba za jadi kwa kukosa fedha kwenda wilayani umbali wa kilometa 56’’.
Na Ibrahim Yassin, Songwe
Diwani wa kata ya Bara iliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe aliyeshika nafasi hiyo toka 1988 hadi sasa Chief Aloyce Mdala vuma amewapongeza wananchi wa kata hiyo kwa kuendelea kumuamini na kushirikiana kuleta maendeleo katika kila sekta.
Amesema yeye ni familia ya Kichifu ambapo mwaka 1972 alite uliwa kuwa barozi wa nyumba kumi wakati huo waliwajibika kwenye serikali wakilipwa posho,mwaka 1983 akiwa kiongozi wa umoja wa ccm,ilipofika mwaka 1987 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kijiji.
Anasema baada ya kufanya kazi kwa uaminifu na utiifu alichag uliwa kuwa diwani lakini aliacha udiwani baada ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa chama kikuu cha ushirika na mwaka 1988 ambapo alitumikia pia kwenye bodi ya kahawa.
Anasema baada ya kutimika katika nafasi hizo mwaka 2000 alichaguliwa tena kuwa diwani wa kata hiyo ya Bara ambapo anawatumikia wananchi hadi sasa huku akijivunia maendeleo lukuki katika kila sekta na kujikita zaidi kwenye kilimo cha Kahawa.
Anesema wakati mkoa wa Mbeya umemegwa na kuuanzishwa mkoa wa Songwe mwaka 2016 aliteuliwa na chama kukaimu nafasi ya mwenyekiti wa ccm mkoa wa ambapo alitumika hadi alipochaguliwa mwenyekiti mpya.
Chief Mdalavuma anasema katika kipindi chote cha udiwani kauli mbiu yake ilikuwa ni elimu afya na maji,ambapo amefani kiwa kujenga shule za msingi katika vijiji vyote Zahanati 4 na shule mbili za sekondari na moja iliyopo kijiji cha Itaka kuipandi sha hadhi kuwa High School wakijenga majengo 4 mapya.
Anasema mbali na hilo pia amefanikisha kujenga barabara na kuzikarabati chakavu na kuzifungua mpya,na kujenga kituo cha afya ambacho ujenzi wake bado unaendelea nakuwa ni kata ya mfano kimaendeleo kwa wilaya ya Mbozi.
Anasema sababu ya kujenga zahanati kila kijiji ni kunusuru wazee na akina mama wajawazito waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kwenda kutibiwa wilayani kilometa zaidi ya 56 huku wengine walitibiwa kwa waganga wa tiba za jadi kutokana na ukosefu wa fedha kwenda wilayani.
‘’Ndugu mwanahabari,ujenzi wa zahanati hizi na kuzifungua barabara za vijiji vyote umepunguza hadha kwa wananchi waliokuwa wakipata shida kutembea umbali wa kilometa 56 hadi wilayani kupata tiba na kukumbwa na changamoto lukuki ikiwemo kujifungulia njiani’’anasema Mdalavuma.
Anasema kutokana na hilo,Rais mtaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete katika utawala wake alifika kwenye kata hiyo na kuifungua shule ya Itaka ambapo baadae waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye nae aliwahi kufika na kuikagua miradi iliyopo kwenye kata hiyo.
Anasema malengo makubwa yaliyopo kwa sasa ni kukamilisha kituo cha afya,High School na barabara ya Lami,na kwmba anajivunia kufanya kazi na marais wote waliopita huku na sasa yupo na Rais Dkt,Samia ambaye anaona kazi kubwa ya maendeleo ikifanyika.
Anasema wakati nchi ikiitwa Tanganyika alikuwa mtu muadilifu kila kitu kinachofanyika alikuwa akidai lisiti na kuzitunza amba po aliweza kuonesha lisiti ya mwezi Juni 24/1946.
Anasema mbali na kujikita katika kazi za kijamii pia anajishugh urisha na kilimo cha Kahawa ambapo tayari amepanda miche 100.000 ya mbegu chotora ya Compact ambayo haishambu liwi na wadudu huku akishirikiana vyema na watafiti wa mbegu kutoka taasisi ya TAcRI.
Asifiwe Mwashilindi mkazi wa bara,anasema diwani Chief Mdalavuma ni moja ya viongozi makini aliyefanikisha kugusha kila idara na kuifanya kata hiyo kuwa ya mfano kimaendeleo ukichukulia wapo pembezoni mwa wilaya.



Comments
Post a Comment