RPC Songwe amtembelea mzee Mkisi Mwalimu mstaafu wa chio cha Polisi Moshi
Na Ibrahim Yassn, Songwe
IMEELEZWA kuwa jamii nchini inatakiwa kujenga utamaduni wa kuwaenzi wazee ili kuwatia moyo kutokana na kazi kubwa waliyoifanya ya kulitumikia Taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 3,2024 na kamanda wa polisi mkoani Songwe Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Augustino Senga wakati akizungumza na Dira Kamilifu.
Amesema wazee ni dhahabu hivyo ukiwepo utaratibu wa kuwatembelea na kupokea ushauri wao mambo yatakwenda vyema huku baraka zikitawala katika mioyo.
Kamanda Senga amesema yeye ni muumini wa kufanya hivyo na anajisikia fahari kuwatembelea wazee waliomtangulia huku akipokea mawazo na ushauri unaomsaidia kuongeza uwajibikaji uliotukuka.
"Najisikia fahari ninapozungumza na wazee kupokea mawazo yao na kuyafanyia kazi, siku ya Agosti 31 mwaka huu nilienda kumtakia hali mzee Mkisi na kupokea mawazo mbalimbali kutoka kwake, ni vyema tukajenga utaratibu huu tuwape faraja wazee wetu"amesema.
Hata hivyo kamanda Senga aliongozana na Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Gallus Hyer walimtembelea Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Emsoni Mkisi.
Mzee Mkisi ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi (CCP) ambaye kwa sasa amestaafu utumishi kwa mujibu wa sheria.
Kamanda Senga akiwa na ACP Hyera walifika nyumbani kwa Mstaafu huyo Kata ya Igamba wilayani Mbozi kwa lengo la kumjulia hari ikiwa pamoja na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo usalama.



Comments
Post a Comment