TEHAMA WATAKIWA KUDHIBITI MIFUMO YA KAMERA.



Na Ibrahim Yassin.Rukwa

MWENGE wa uhuru umeweka jiwe la msingi la uwekaji wa kamera za CCTV za utoroshwaji wa mapato katika Kijiji cha Mwimbi kata ya Mwimbi wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa zitakazosaidia kudhibiti utoroshwaji wa mapato yatokanayo na mazao katika halmashauri hiyo.

Akizungumza jana kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Godfrey Mnzava alisema ni wakati sasa wataalamu wa tehama kuhakikisha wanaendelea kudhibiti mifumo hiyo pamoja na kukomesha vitendo vya watu wanao haribu mifumo hiyo.

" Niwatake tehama hakikisheni hakuna anaeingilia mifumo ya kamera maana teknolojia inavyokuwa hata wasiyoitakia mema nchi yetu nao wanajaribu kuendana na teknolojia hiyo"amesema Mnzava.

Wakati huo huo Tsh, milioni 436,567,205 zimetatua kero ya maji katika kijiji cha Kalaela kata ya Nsundu wilaya ya Kalambo kwa ujenzi wa tanki la maji utakao hudumia kaya zaidi ya 2000 wa kijiji hicho.


Akizungumza kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava aliwataka wananchi kutunza miundombinu hiyo na kuendelea kuchangia fedha za uendeshaji wa miradi ya maji.

Aidha amesema serikali inalenga kuwasaidia wananchi kwa kutatua changamoto zao ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya huduma za jamii.

 Dwani wa kata ya Nsundu Peter Simuyemba  amemshukuru Rais Dk, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha ambazo zimejenga tanki la maji na mradi huo umekuwa mkombozi kwa wakazi wa kijiji hicho.



Pia wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwazye wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa mabweni katika shule hiyo ambayo yatasaidia kupunguza utoro na kuongeza ufahuru shuleni hapo.

Wamesema wataendelea kusoma kwa bidii ili kumuunga mkono Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazozifanya za kujenga na kukaraba ti miundombinu ya Elimu.



Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuacha vitendo viovu visivyokuwa na maadili na kuwataka kutumia majengo hayo kwa manufaa ya kufikia ndoto zao.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa