Miradi ya Tarura Na Ruwasa ilivyomkosha kiongozi wa mbio za Mwenge mkoani Songwe


Na Ibrahim Yassin,Songwe

KIONGOZI wa mbio za Mwenge kitaifa Godfrey Mzava amekoshwa na usimamizi mzuri uliotukuka katika miradi ya maji inayotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Ruwasa ) na wakala wa barabara vijijini na mijini (Tarura) ambapo mameneja wa taasisi hizo wametwa kuzitendea haki fedha za serikali.

Mzava katika ukaguzi wa miradi hiyo akianzia wilayani Songwe aliridhishwa na ujenzi wa mradi wa maji uliokuwa ni kero ya muda mrefu katika kata ya Kanga baada ya serikali kutoa Milioni 144 kujenga mradi ambao umetajwa kuwa ni muoarobaini kwa wakazi wa eneo hilo.



Kutokana na kero hiyo ya muda mrefu kwa wakazi wa vijiji vitatu imetatuliwa baada ya Serikali kutoa Tsh, 144.040,799.33 kujenga mradi huo kumaliza changamoto hiyo.

Meneja wa mkoa anayesimamia taasisi ya maji safi na usafi wa mazingira (Ruwasa) Mhandisi,Charles Pambe na meneja wakala wa barabara mijini na vijijini Tarura Mhandisi Kilian Haule pamoja na mameneja waliopo wilayani wametajwa kufanya kazi vizuri katika usimamizi wa miradi hiyo.



Comments