KIONGOZI WA MBIO MWENGE AAGIZA UJENZI WA DARAJA MTO ISENGA UHARAKISHWE NA UBORA UZINGATIWE.



Na Ibrahim Yassn Songwe. 

WANANCHI kata ya Chitete Wilayani Ileje Mkoani Songwe wataondokana na adha ya kivuko katika mto Isenga Ikumbilo ambao unaunganisha vijiji zaidi ya  7 kutokana na ujenzi wa daraja la kudumu kujengwa ambalo linatarajiwa kumalizika Januari 2025 .

Kwa muda mrefu wananchi walikuwa wakikumbwa na kadhia hiyo hasa nyakati za mvua za masika lakini serikali ya awamu ya sita imepeleka fedha kujenga daraja hilo.

Elizabeth Kandonga mkazi wa Ikumbilo amesema  kukamilika kwa daraja hilo wataondokana na adha iliyopo hasa kipindi cha mvua kutokana na mto huo kujaa maji huku daraja hilo likisababisha wananchi kusombwa na maji na wengine kupote za maisha.



Gordon Kibona mkazi wa Chitete amesema Daraja hilo litakuza uchumi kwani vijiji 7 ambavyo vilikuwa vikikosa mawasiliano nyakati za mvua sasa vitafunguka 

Wananchi hao wameyasema hayo leo September 4/2024 wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kati ka daraja hilo ambalo linagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 447 likisimamiwa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura).

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa daraja hilo Meneja wa Tarura Wilaya ya Ileje Mhandisi Lugano Mwambingu amesema kukamilika kwa daraja hilo linakwenda kutatua changamoto na kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Mnzava mara tu baada ya kuweka jiwe la msingi amepongeza hatua ya ujenzi iliyofikia na kuwataka Tarura kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati.

Amesema kutokana na umuhimu wa daraja hilo ujenzi uharakishwe  bila kuathiri viwango na ubora unaotakiwa ili liweze kudumu kwa muda mrefu na kuwaondolea adha wananchi.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa