MADIWANI NKASI WATAKIWA KUWA CHACHU YA UKUSANYAJI WA MAPATO
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
Madiwani wa halmashauri ya wilaya Nkasi wametakiwa kuongeza nguvu ya usimamizi Kwa Maafisa Watendaji wa kata zao kuhakikisha kwamba Kasi ya ukusanyaji wa mapato inaongezeka.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Nkasi Pankrasi Maliyatabu kwenye kikao Cha Baraza la Madiwani Leo ambapo amedai kuwa Moja ya jukumu lao kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ni pamoja na suala la Zima la kuhakikisha katika maeneo Yao makusanyo ya halmashauri yanapatikana.
Amedai kuwa Ili halmashauri iweze kupata uwezo wa kushughulika na uendelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo Yao ni lazima fedha iwepo na hili kuweza kufanikisha katika Hilo ni lazima kuwepo na makusanyo,hivyo ni lazima kila Mmoja aone kwamba ukusanyaji wa mapato ni jukumu lake Kwa kuwasimamia na kutoa ushirikiano wa kutosha Kwa Watendaji wao.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Afraha Hassan Kwa upande wake amedai kuwa suala la upotevu wa mapato Kwa Watendaji wa kata amelipata na kuwa kufuatia hari hiyo akizungumza nao na na kuwekeana mikakati na kuwa Sasa kila mwisho wiki kila Mtendaji wa kata atakua anatoa taarifa ya mapato katika kata yake.
Amesema kuwa pia ataendelea kufanya vikao na Maafisa Watendaji wa kata vya mara Kwa mara Ili kuhakikisha kwamba mapato yanapatikana katika maeneo Yao na kuwezesha halmashauri kufikia malengo ya makusanyo na hata ikibidi kuvuka lengo.
Awali afisa serikali za mitaa mkoani Rukwa Vaileth Shirima Kwa upande wake amewataka Madiwani na Watendaji wa halmashauri kuhakikisha kwamba wanatoa ushirikiano wa kutosha Kwa mkurugenzi mtendaji ambaye ni mgeni na kuwa hiyo ndiyo itakuwa jawabu la kuyafikia maendeleo wayatakayo.
Amesema kuwa wakati huu usiwe muda wa kupeana lawama na kulaumiana bali uwe ni muda wa kujipanga na kubwa ni kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato na kuwa halmashauri Ili iweze kuwahudumia Wananchi wake vyema ni lazima makusanyo ya kutosha yawepo na kulifikia Hilo ni lazima uwepo ushirikiano wa kutosha.
Baraza la Madiwani Leo lilikua katika siku yake ya kwanza ambayo ni kupokea taarifa mbalimbali za kata



Comments
Post a Comment