Mwenge walidhishwa na miradi ya Tarura na Ruwasa Songwe



Na Ibrahim Yassin,Songwe

KIONGOZI wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mzava amekoshwa na usimamizi mzuri uliotukuka katika miradi ya maji inayotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Ruwasa ) na wakala wa barabara vijijini na mijini (Tarura) ambapo mameneja wa taasisi hizo wamepongezwa kuzitendea haki fedha za serikali.

Mzava katika ukaguzi wa miradi hiyo akianzia wilayani Songwe aliridhishwa na ujenzi wa mradi wa maji uliokuwa ni kero ya muda ya mrefu katika kata ya Kanga baada ya serikali kutoa Milioni 144 kujenga mradi ambao umetajwa kuwa ni muoarobaini kwa wakazi wa eneo hilo.



Kutokana na kero hiyo ya muda mrefu kwa wakazi wa vijiji vitatu imetatuliwa baada ya Serikali kutoa Tsh, 144.040,799.33 kujenga mradi huo kumaliza changamoto hiyo.

Mbali na mradi huo mradi mwingine ulizinduliwa wilayani Momba ambapo kiongozi huyo aliridhishwa kwa usimamizi uliotukuka na baada ya hapo siku iliyofuata mwenge ulienda wilayani Mbozi na ukakagua mradi wa maji Ukwile.

Mradi huo wa Ukwile unaosaidia watu zaidi ya 7.000 wa vijiji vilivyopo kata ya ukwile wilaya ya Mbozi ambao tayari wameanza kunywa maji safi na salama baada ya miaka 40 tangu kijiji hicho kianzishwe mwaka 1980,

Jambo hiii limefahamika jana baada ya mwenge wa uhuru kuzindua rasmi mradi wa maji katika kijiji cha chimbuya uliogharimu zaidi ya shingi million 500,Pia ukakagua mradi wa maji Msia wa Bilioni 1.1 ambapo aliridhishwa na utekelezaji wake,baada ya hapo ulimalizia Halmashauri ya mji Tunduma nako aliridhishwa.




Baaada ya kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo ya maji pia Mwenge huo ulikagua miradi ya miundombinu inayotekelezwa na TARURA ukiwemo wa Chango’mbe kiongozi huyo wa mbio za mwenge aliridhishwa na kusifu utekelezaji wa miradi hiyo.

Licha ya kiongozi huyo wa mbio za mwenge Godfrey Mzava kupongeza utekelezaji wa miradi ikiwemo ya RUWASA NA TARURA,alisisitiza mfumo wa NeST utumike katika manunuzi na pia aliweza kushauri pale palipoonekana pana kasoro.

Hata hivyo baadhi ya wananchi katika halmashauri hizo walisifu usimamizi mzuri wa mamaneja wa taasisi hizo mbili wakidai wameuheshimisha mkoa kwa utekelezaji na usimamizi wa miradi hiyo ikiwemo nidhamu ya matumizi ya fedha.



Leo Septemba 5/2024 mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo ameukabidhi mwenge huo kwa mkuu wa mkoa wa Rukwa baada ya kumaliza ukaguzi katika halmashauri zote za mkoa wa Songwe mwenge huo ukiwa salama leo hii utaanza rasmi kuzunguka kwenye miradi iliyopo mkoani Rukwa

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa