Kijiji chapata maji toka kianzishwe mwaka 1980, Wananchi wafurahia
Na Ibrahim Yassin,Songwe
Zaidi ya wananchi 7.000 wa vijiji vilivyopo kata ya Ukwile wilaya ya mbozi mkoani Songwe wameanza kunywa maji safi na salama baada ya miaka 40 tangu kijiji hicho kianzishwe mwaka 1980 .
Jambo hili limefahamika jana baada ya mwenge wa uhuru kuzindua rasmi mradi wa maji katika kijiji cha chimbuya uliogharimu zaidi ya shingi million 500.
Ester Mbwete mkazi wa Chimbuya amesema ana kila sababu ya kuipongeza serikali kwa kukamilisha mradi huo kwani wataondokana na homa za matumbo kwani toka mwaka 1980 kijiji kilipoanzishwa hawakuwahi kuwa na huduma hiyo.
Happiness Mgetta mkazi wa Chumbuya amesema wakati mradi huo unaanzishwa waliona ni kama ndoto lakini tayari mradi umekamilika na kuzinduliwa na Mwenge wa uhuru hivyo anaipongeza serikali kukam ilisha mradi huo.
"Wakati mradi unaanzishwa wahandisi kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira walikuwa wanafika mara kwa mara kufuatilia mradi huu hadi leo tunakunywa maji safi , ni jambo la kumshukuru Mungu" amesema Mgetta.
Nae Ekson Msolo mkazi wa Chimbuya amesemai kuwa kabla ya mradi huo kujengwa walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata maji huku mifugo yao ikikosa sehemu ya kunywa hali iliyopelekea kuwa na afya mbovu.
Akisoma taarifa ya mradi huo meneja wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira (RUWASA) wilaya ya mbozi mhandisi Ismail Ismail amesema utekelezaji wa mradi huo ulianza February 17 mwaka jana.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Godfrey Mzava baada ya kuukagua mradi huo na kuona upo vizuri alitoa rai kwa viongozi wilayani humo kutumia mfumo wa NeST katika manunuzi ili kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza



Comments
Post a Comment