Kayogolo achaguliwa tena kuwa Makamo Mwenyeki halmashauri Nkasi



Na Israel Mwaisaka,Nkasi

BARAZA la Madiwani wa halmashauri ya wilaya Nkasi limemchagua Stephen Kayogolo kuwa makamo mwenyekiti wa halmashauri.

Madiwani hao Kwa kauli Moja walitoa tamko la Kayogolo kuwa makamo mwenyekiti akiwa ni mgombea pekee kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo CHADEMA wao hawakupeleka mgombea kwenye kinyang'anyiro hicho.


Pia Nestory Kaloto diwani wa kata ya Namanyere amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira na Carolina Makandi diwani wa kata ya Paramawe amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Elimu,Afya na Maji.

Kayogolo Kwa upande wake amewashukuru Madiwani wenzie Kwa kumpa kura zote na kuwa Imani waliyokuwa nayo Madiwani wenzie kwake atahakikisha atawatumikia vema katika nafasi hiyo Kwa kumshauri mwenyekiti wa halmashauri vyema Ili kuweza kuyafikia malengo.

Mwenyekiti wa halmashauri Pankrasi Maliyatabu Kwa upande wake amewataka Madiwani kuendeleza kazi kubwa waliyoianza ya kuhakikisha halmashauri inaongeza makusanyo yake kwa kuwasimamia vyema Maafisa Watendaji wa kata Ili kila Mmoja awajibike katika eneo la makusanyo.


Mkurugenzi mtendaji halmashauri Afraha Hassan yeye amewaomba Madiwani kutoa ushirikiano wa dhati Kwa kuhakikisha suala la makusanyo ya halmashauri linapewa kipaumbele na kuwa amewaona Madiwani wote kila Mmoja ana Nia ya dhati katika kufanikisha Hilo na kuwa wao kama Watendaji wa halmashauri nao watatoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha lengo Hilo linafikiwa.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa