Mradi wa maji wa Mil.144 wazinduliwa na mbio za Mwenge



Na Ibrahim Yassin,Songwe

KERO ya muda ya mrefu ya uhaba wa maji kata ya Kanga wilayani Songwe mkoani hapa imepatiwa majibu baada ya serikali kutoa Milioni 144 kujenga mradi ambao umezinduliwa na mbio za mwenge.

Kutokana na kero hiyo ya muda mrefu kwa wakazi wa vijiji vitatu imetatuliwa baada ya Serikali kutoa Tsh, 144.040,799.33 kujenga mradi huo kumaliza changamoto hiyo.



Akizungumza jana mbele ya mkimbiza mwenge kitaifa ,Mkuu wa wilaya hiyo Solomon Itunda alisema kwa muda mrefu wananchi walipata shida kwa kukosa maji safi lakini serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt, Samia imesikia kilio chao na kuwafuta machozi.

Alisema serikali imemtua mama ndoo kichwani baada ya kero ya muda mrefu kwani Rais Dkt.Sam ia amekuwa msikivu na anajali shida za wananchi hivyo aliwataka wananchi kuutunza mradi.

Akizungumzia mradi huo meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira (RUWASA) wilayani Songwe Boniface Mfungo alisema mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Tsh, 488.930,43 7.64.

Alisema mradi wa maji Galula utasaidia wakazi wa vijiji vya Ilasilo, Kanga na Galula ambapo hadi sasa una wateja wa majumbani 92 kati ya hao 23 wametokea kijiji cha Ilasilo.

Alisema mradi huo utasaidia wakazi 12.657 wa vijiji hivyo ambao mtandao usambazaji maji ni mita 5.640 na mtandao bomba kuu ni mita 12.920..

Mbunge jimbo la Songwe Philipo Mulugo alisema ana kila sababu ya kumpongeza Rais kwa usikivu wake huku akiwataka wananchi kutoharibu miundombinu hivyo ili iweze kuwasaidia wao na vizazi vijavyo .



Godfrey Mzava kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa licha ya kupongeza na kuufungua mradi huo alisema jambo la muhimu ni kuzingatia mfumo wa NeST kwenye manunuzi na kumpata mkandalasi anayefaa kwa njia sahihi.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa