WADAU WATOA YA MOYONI WAKIKOSHWA NA MIRADI YA RUWASA NA TARULA-RAIS SAMIA-RAS SENEDA WATAJWA.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
SIKU chache baada ya mwenge wa uhuru kufika na kukagua miradi ya maendeleo hususani miradi muhimu ya miundombinu ya barabara na madaraja na ile ya maji,wananchi wametoa ya moyoni baada ya miradi hiyo kumkosha mkimbiza mwenge kitaifa.
Mkoa wa Songwe ni moja ya mikoa mipya nchini uliomegwa kutoka mkoa wa Mbeya Octoba 18/2015 ikiwa na wilaya 4 na halmashauri 5 yaani Ileje,Momba,Tunduma,Mbozi na Songwe na wilaya 4 ambazo ni Momba,Songwe,Ileje na wilaya mama ya Mbozi.
Mkoa una kata 94,vijiji 307 huku ikiwa na wakazi 1.344,687 kati ya hao wanaume ni 643,679 wanawake ni 701,008 ambapo idadi kubwa ya wakazi ni wakulima na wafugaji,hii ni kwa mujibu wa sense ya watu na makazi.
Kwa mwaka 2022/23 Rais Dkt,Samia alitoa Tsh,Bilioni 20.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara,na mwaka 2023/2024 alitoa Bilioni 17,
Kwa upande wa miradi ya maji Rais Dkt,Samia mwaka 2023/24 baada ya kutoa fedha wakala ulipanga kutekeleza jumla ya miradi 1,546 katika mikoa 25 nchini ikiwemo Songwe,iliyogharimu Tshs,500,342,398,033.25.
Miradi hiyo inategemewa kuhudumia watu wapatao 2,274,193 katika vijiji 844 na katika kipindi cha nusu mwaka wa 2023/24 hadi kufikia Disemba 31/2023 jumla ya miradi 374 iliyogharimu Tshs,128,177,655,8 82 ilikuwa imekamilika.
Aidha mwaka wa 2024/25 kuna fedha nyingi zimetolewa kutekeleza miradi hiyo nchini na mkoa wa Songwe ukiwa mnufaika ambapo hadi sasa hali ya upatikanaji wa maji ni zaidi ya asilimia 78 huku jitihada zaidi zikifanyika kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na maji safi na salama,
Asilimia 75 ya wakazi wa mkoa huo utegemea kilimo na ufugaji na uvuvi kuendesha maisha yao ya kila siku huku wakiwa na uhitaji mkubwa wa miundombinu ya barabara na madaraja kusafirisha bidhaa zao kwenda kwenye masoko mikoani huku uhitaji wa maji safi na salama ukiwa ni mkubwa zaidi.
Miaka mitatu ya nyuma wakazi wa mkoa wa Songwe hasa watokao maeneo ya bonde la Kamsamba walikuwa wakitaabika kutokana na ukosefu wa barabara na madaraja hali iliyowalazimu kuuza mazao yao kwa bei ya chini kutokana na kushindwa kusafirisha mazao yao.
Kwa upande wa maji wengi wao walitumia maji ya kwenye mito,mifereji na ya kwenye madimbwi ambayo hayakuwa safi na salama hali iliyosababisha baadhi waugue magonjwa ya milipuko hasa kwa wilaya ya Songwe ambao watu walikumbwa na kipindupindu kwa kunywa maji yasiyofaa.
Kutokana na changamoto hiyo,viongozi ngazi ya wilaya na mkoa walipigania upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na miundom binu ya barabara na madaraja huku wabunge wa majimbo yote wakiwa Bungeni walilazimika kuomba kujengewa miradi hiyo kuwaondolea wananchi changamoto hizo.
Katika awamu ya 6 chini ya Rais Dkt,Samia Suluhu miradi ilianza kuje ngwa baada ya serikali kupeleka fedha kujenga miradi kuwaondolea changamoto wananchi ambapo karibu vijiji vyote tayari vimewekewa maji na hata miundombinu ya barabara kwa sasa ipo vizuri japo sio za kiwango cha Lami lakini zinapitika.
Ujio wa fedha hizo zilipelekea viongozi ngazi ya wilaya na mkoa kuipitia na kuikagua miradi hiyo kuhakikisha inajengwa kwa kufuata viwango na nidhamu ya fedha na ilikamilika kwa viwango stahiki hali iliyopelekea hata kiongozi wa Mbio za mwenge kuisifu.
Katibu tawala mkoani Songwe Happiness Seneda alilazimika kufanya ziara kata kwa kata katika mkoa mzima kuipitia miradi inayotekelezwa ikiwemo ya maji na miundombinu ya barabara na madaraja ambapo alikuwa mkali pale alipoona changamoto katika utekelezaji wake na alishauri pale alipoona pana udhaifu.
Wiki 2 zilizopita mwnge wa uhuru ulifika mkoani Songwe na kukagua miradi mbalimbali iliwemo ya maji na barabara katika halmashauri zote ambapo miradi hiyo ilionekana kujengwa kwa kufuata utaratibu na imeonekana kuwa ni mizuri licha ya kuwa kiongozi wa wa Mbio za mwenge Godfrey Mzava kuagiza mfumo wa Nest utumike katika manunuzi.
Asifiwe Mtafya mkazi wa Ileje alisema ana kila sababu ya kumponge za Rais Dkt,Samia kwa moyo wa upendo kwani katika utawala wake fedha nyingi za miradi zilipelekwa mkoani Songwe na katibu tawala Happiness Seneda na timu yake ya mkoa walifanya ziara za kata kwa kata kuipitia miradi yote kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango.
Mambo Mwashilindi mkazi wa Songwe,anasema wilaya ya songwe imefunguka katika utawala wa Rais Dtk,Samia kwani kila Kijiji kina barabara na maji safi na hata homa za kipindupindu kwa sasa hazipo hivyo wana kila sababu ya kumshukuru Mh,Rais,na pia uongozi wa wilaya na mkoa hawakulala walipita kila palipo na mradi kuona changamoto.
Secilia Sichalwe mkazi wa Momba,anasema miaka 3 ya nyuma walikuwa hawaoni faida ya kilimo kutoka na na miundombinu ya madaraja na barabara kuwa ni mibovu,lakini kwa sasa barabara zimejengwa wameweza kukuza pato lao kwa kusafirisha mazao yao kwenda mikoani na hata wanunuzi wakubwa wanafika na magari yao pasina shaka.
Nae Samwel Simbeye mkazi wa Mbozi,anasema kwa upande wa maji na barabara Rais kauheshimisha mkoa wa Songwe na hata wahusika yaani Ruwasa na Tarura wamezitendea haki fedha za serikali kwani miradi ni mizuri kazi iliyopo ni kuitunza ili isaidie hadi vizazi vijavyo.
Kilian Haule meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini (RUWA SA) mkoani humo, anasema siri ya mafanikio ushirikiano kati ya vion gozi wa wilaya na mkoa na kwamba ufuatiliaji na kuwasimamia waka ndarasi kufuata vigezo vya ujenzi nayo ni sababu kupelekea miradi kujengwa na kukamilika kwa wakati na viwango.
‘’Ndugu mwanahabari Serikali ya wamu ya sita chini rais Dkt,Samia imefanya kazi kubwa,hivi sasa kila Kijiji kinapitika barabara zimejengwa japo sio za Lami lakini hata nyakati za mvua zinapitika,wakulima wameongeza vipato vyao na mkoa umefunguka’’anasema Mhandisi Haule.
Charles Pambe meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Ruwasa) mkoani humo,anasema fedha za miradi zinapokuja wakandarasi wa kampuni za ujenzi wanapotekeleza miradi hiyo wanakuwa wakuwafuatilia kwa karibu kuona kama viwango stahiki vinatumika katika ujenzi hali inayopelekea miradi kuamilika vizuri.
‘’Serikali ya Rais Dkt,Samia imefanya kazi kubwa, katika utawala wake karibu kila Kijiji kina huduma ya maji safi na salama hali iliyopunguza ama kuondoa kabisa homa za matumbo hasa kipindupindu,kazi iliyobaki ni kwa wananchi kuvuta bomba kwenye kaya zao na kuilinda miundombinu’’anasema Mhandisi Pambe.







Comments
Post a Comment