Mapokezi ya Mwenge wa uhuru Songwe ulivvyoleta shangwe kwa Wananchi
Na Ibrahim Yassin,Songwe.
MAAFISA, wakaguzi na askari wa vyeo mbali mbali wakidumisha ulinzi na usalama katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru uliopokelewa Kijiji cha Ifwenkenya wilayani Songwe mkoani Songwe tarehe 31 Agosti, 2024.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Happyness Seneda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo amepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoa wa Mbeya.
Seneda ameeleza kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Songwe utakimbizwa Kilomita 634.2 kati ka wilaya 4 na halmashauri 5 za na utatembelea, utakagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maen deleo 46 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 18.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa katika uwanja wa Shule ya Msingi Ifenkenya wilaya ya Songwe tayari ukiwa salama kwa ajili ya kukimbizwa Mkoani humo.
Mwenge huo utaanza halmashauri ya Songwe,Mo mba,Mbozi Ileje na Tunduma huku kila halmashau ri ikifanywa maandalizi ya kutosha kuhakikisha mambo yanaenda sawa.
Wananchi kwa upande wao
wameungana na viongozi mbalimbali kuhudhuria mapokezi hayo na kutoa ushirikiano mzuri




Comments
Post a Comment