TUTUNZE MAZINGIRA KWA TAIFA ENDELEVU.



Na Ibrahim Yassn Rukwa

ZAIDI ya Milioni137  zitatumika kutengeneza vitalu vya miti katika hifadhi ya msitu wa mbizi kwa lengo la kupata miche itakayopandwa na taasisi mbalimbali kwa ajili ya uboreshaji wa mazingira katika mkoa wa Rukwa.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo muhifadhi mkuu wa msitu wa mbizi (TFS) katika halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga Egnasi Lupala amesema zaidi ya miti laki nane imepandwa ikiwa mradi huo unalengo la kuotesha miche milioni moja na laki mbili na hamsini kwa lengo la kuhifadhi mazingira.

"Msitu wa mbizi unaekali 14.7 ili kuendeleza uhifadhi wa mazingira tunalengo la kupanda miti milioni moja na laki mbili na hamsini na mpaka sasa tumefanikiwa kupanda kuotesha miche laki nane .



Naye kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava amesema serikali inaunga mkono jitihada zina zofanywa na taasisi binafsi katika suala la kukuza maendeleo ya nchi.

Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki cha Alpha Tanganyika Fravour Limited amesema serikali inataka kuona wananchi wanapata maendeleo makubwa kwa kuanzisha taasisi mbalimbali ili kuongeza upana wa ajira kwa vijana.

Aidha ameitaka halmashauri kuhakikisha wanashirikiana na mmiliki huyo katika kutatua changamoto za kiwanda namna ya upatikanaji wa malighafi na utoaji wa vibari na utoaji wa Elimu hiyo.

kiwanda cha kuchakata minofu ya samaki cha Alpha Tanganyika Fravour Limited kimetajwa kuongeza ajira na fursa za kuichumi.

Aidha mwenge wa Uhuru pia umekagua ujenzi wa majengo manne (4) katika hospitali ya manispaa ya Sumbawanga ujenzi uliyo gharimu fedha shilingi 923,771,184.04 katika hospitali hiyo.

Ujenzi wa majengo manne ya hospitali ya manispaa yamejengwa kwa fedha kutoka serikali kuu ambapo majengo matatu yapo katika hatua ya umaliziaji ambayo ni maabara,stoo ya dawa na jengo la mionzi ambayo yamejengwa kwa gharama ya sh.200,000,000.00 pamoja na ujenzi wa jeng o la kuhifadhia maiti.

Akizungumza jana  baada ya kukagua majengo hayo kiongozi wa mwenge kitaifa Godfrey Mnzava amesema serikali inafanya jitihada ya kuhakikisha miradi ya huduma za kijamii inakamilika kwa wakati na wananchi wanaendelea kupata huduma.

Mwenge wa Uhuru umeendelea na mbiyo zake mkoani Rukwa ambapo leo umekimbizwa katika halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kuzindua, kukagua miradi ya maendeleo na uwekaji wa mawe ya msingi katika miradi 11 yenye thamani ya fedha Tshs, 10.535..441.670.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa