Uongozi wa Rais Samia waing'arisha Kyela kwa maendeleo lukuki


Na Ibrahim Yassin. Kyela

IMEELEZWA kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameweka historia ya kimaendeleo Wilayani Kyela Mkoani Mbeya.

Hayo yamebainika baada ya Dirakamilifu kuongea na madiwani pamoja na wadau wa Maendeleo Wilayani humo ambapo wamesema Wilaya ya Kyela imekumbana na mabadiliko makubwa ya Kimaendeleo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Elia Mwaipetania Diwani wa Kata ya Ipinda ameeleza kuwa tangu aingie madarakani kama Diwani amekuwa akifanya kazi zake kirahisi kutokana na uwepo wa Rais Samia kwa kuwapiga tafu kila wanapoomba msaada wa kimaendeleo.

Mwaipetania amesema Rais samia amekuwa akitoa fedha kwa kila Sekta jambo ambalo limepelekea uwepo wa maendeleo ya haraka Wilayani Kyela na kusema kuwa huenda ndiye Rais aliyevunja rekodi ya mageuzi ya kimaendeleo katika wilaya ya Kyela.

Amesema licha ya wilaya hiyo kukumbwa na changamoto za kisiasa kwa miaka mingi kutokana na uwepo wa makundi lakini kwa miaka ya hivi kalibuni kumekuwepo na utulivu mkubwa kwani kila sekta inafanya maendeleo.

Diwani huyo amesema katika sekta ya Afya kwenye Kata yake wameweza kujenga jengo la x-ray katika zahanati ya Ipinda pamoja na ununuzi wa kifaa cha kupimia yaani x-ray.

Wamejenga jengo la Mama na Mtoto pamoja na jengo ya kupumzikia kwa wanaosubiria huduma ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya Mtumishi kwa kushirikiana na Wananchi pamoja na mdau.

Kwa upande wa elimu Diwani huyo amesema kuwa wameweza kujenga vyumba nane vya madarasa kwa shule ya msingi Mwenge,Matundu sita ya Vyoo, vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Lupaso, vyumba 4 shule ya Mabunga, vyumba 2 shule ya Kafundo, vyumba 4 katika shule ya Kanga na Vyumba 4 vya madara shule ya Ikulu.

Aliongeza kuwa katika shule ya Jitegemee wamejenga vyumba 4 na ukarabati wa majengo chakafu katika shule ya Ikulu na ujenzi wa matundu 22 ya vyoo vya kisasa katika Shule ya Kisale pamoja na ujenzi wa kisima cha maji safi kilichojengwa na mdau wa Maendeleo.

Mwaipetania amesema kuwa upande wa Miundombinu Ipinda ndio kata pekee iliyokuwa na Taa za barabarani jambo ambalo alisema anajivunia kwa hilo.

Aidha amesema wameweza kujenga ma boksi karavati matano (5) barabara ya Kutoka Ngamanga kitongoji cha Ibenga kwenda Lusungo, kuchonga barabara ya kutoka Kanga – Kingili mpakani mwa Kyela na Busokelo na kuweka kifusi kwenye barabara hiyo kwa kilomita mbili.

Kwa upande wa Maji diwani huyo amesema vijiji vya Kikusya na Matema kulikuwa na shida ya maji lakini mradi wa Million 600 umejengwa katika kijiji cha Ipinda na Kafundo nakuondokana na kero iliyokuwepo.

Aidha amesema kuwa sekta ya umeme ndo Rais Samia amevunja rekodi kwani vijiji vya Ngamanga Kitongoji cha Ibungu, Kisale hadi Kanga kilomita moja umeme umewekwa, Kanga kilomita 3 Ikulu kilomita 8.7 kafundo kilomita 7.8, nakusema kuwa Ipinda wamepewa bei Punguzo ya Umeme wa Rea.



Kwa upande wake Diwani wa Kyela Mjini Andrew Ndomba amesema kuwa awamu ya sita ndiyo imevunja rekodi ya maendeleo kwa kata hiyo kwa ujenzi wa Barabara za Lami karibu kila mtaa wa mjini.

Ndomba amesema kuwa kila Kata za Mjini Kyela zimejengwa barabara kwa kiwango cha lami ambapo kiasi cha Shillingi Billion 1.6 zimetumia kwa urefu wa kilomita zaidi ya 4.

Ameongeza kuwa kata hiyo inaendelea na ujenzi wa makaravati 4 ambapo moja tayari imeshakamilika.

Kwa upande wa Elimu amesema kupitia fedha ambazo zinatolewa na Rais Samia wameweza kujenga vyumba vya madarasa vitatu na matundu 10 kwa shule za Kyela Mjini ambapo kiasi cha fedha Million 66.9 zimetumika.

Aidha amesema kiasi cha fedha shillingi Milion 36 zinajenga darasa la watu maalumu pamoja na vyoo matundu mawili ili na wao wasipate shida katika masomo yao.

Katika sekta ya maji Diwani Andrew amesema kuna mradi mkubwa wa maji kutoka Mbambo unaoghalimu kiasi cha Bilion 4 ambapo amesema maji hayo yatakuja kusambazwa Kyela Mjini nakuondokana na upungufu wa Maji wilayani humo.

Aidha amesema mradi huo tayari umeshaanza na asilimia 65 umeshakamilishwa kwa zaidi ya kilomita 30 za Mjini kwa ajili ya kusambaza maji.

Amesema kwa sasa mipango yao ni kuhakikisha wanaweka Mataa kwenye barabara zote za Mjini ili kuendana na kasi na mvuto wa Muonekano wa Wilaya hiyo.

Pia amesema serikali ina mpango wa kuboresha barabara zote za Vumbi zilizopo kati kati ya mji ili wananchi waendelee kufurahia muonekano wa Wilaya yao chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Hunter Mwakifuna ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyela na Diwani mstaafu wa Kata ya Ipinda amesema kuwa Kyela ya sasa sio Kyela ya zamani chini ya Rais Samia kumekuwepo na utofauti Mkubwa wakimaendeleo hasa kwenye sekta ya Miundombinu.

Mwakifuna amesema awali kulikuwepo na makundi kwa upande wa Madiwani wenyewe kwa wenyewe jambo ambalo lilichangia kwa kiasi kikubwa kudumaza maendeleo ya Wilaya hiyo.

Amesema kila Diwani alipigania upande wake barabara ya kuangalia maeneo ambayo yalikuwa nyuma kimaendeleo ili wilaya iende kwa mfumo mmoja wa kimaendeleo.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa