Waandikishaji wa Wapiga kura waonywa dhidi ya Rushwa
Na Baraka Lusajo,Kalambo
Kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa imetoa tahadhari kwa waandikishaji wa Wapiga kura kujiepusha na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja na kutowaandikisha watu kutoka Nchi za jirani na kusisitiza kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wandikishaji ambao watabainika kukiuka kwa makusudi kanuni za uchaguzi.
Mapema akiongea kupitia mafunzo ya wandikishaji Wapiga kura Wilayani humo, Mkuu wa TAKUKURU Wilayani Kalambo Lupakisyo Mwakyolile akawataka wandikishaji kujiepusha na vitendo vya rushwa wakati wa zoezi hilo na kusema mtu au watu ambao watabainika kujihusiha na vitendo hivyo watachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kifungo cha miaka 20 jela
Mkuu wa idara ya uhamiaji Wilayani humo Bw. Kumbo Shaban Mbwana amesema watu watakao takiwa kujiandikisha kwenye zoezi hilo ni wale ambao ni raia wa Tanzania na kusisitiza wandikishaji kufanya kazi hiyo kwa weledi na kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali.
Katibu tawala Wilayani humo Bw. Serivi Ndumbalo akasisitiza wandikishaji kukiishi kiapo walicho apa ikiwa ni pamoja na kuzingatia utuzaji wa siri na kuimalisha ushirikiano wakati wa utekezaji wa majuikumu yao.
Zoezi hilo linafanyika kwa muda wa siku mbili likiwa na lengo la kutoa mafunzo kwa wandikishaji wa orodha ya wapiga kura ambapo waandikishaji 422 Wameshiriki kwenye mafunzo hayo.



Comments
Post a Comment