CHMT SONGWE NA MKAKATI WA KUZUIA MAGONJWA YA MLIPUKO
Na.Ibrahim Yassin. Songwe
Mkuu wa Wilaya ya Songwe,Mhe. Solomon Itunda amefanya kikao na Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya (CHMT) Wilayani humo kujadili masuala ya kiafya ikiwemo namna ya kuzuia magonjwa ya mlipuko katika Wilaya hiyo.
Mhe. Itunda amekutana na timu hiyo mwanzoni mwa wiki hii katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Songwe iliyopo Mkwajuni huku akiiagiza timu hiyo kuhakikisha wanasimamia usafi wa mazingira na kila kaya kuwa na vyoo bora.
Amesema kuwa kaya na maeneo yanayotoa huduma ambayo hayana vyoo bora wanaohusika wachukukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria zilizopo.
"kumekuwa na kawaida kwa baadhi ya kaya kuwa na vyoo hatarishi kwa afya , tunataka ujenzi wa vyoo bora vyenye maji tiririka ili kuepuka magonjwa ya milipuko"amesema Dc Itunda.
Mganga mkuu wilayani humo Dkt.Carvin Mwasha amesema wamejipanga vizuri kutimiza agizo la mkuu wa wilaya kwani timu yake ya wataalamu itahakikisha kila kilichopangwa kinafanyika kiufasaha.
"Afya za wananchi ni muhimu kwani shughuri za uzalishaji mali na ujenzi wa Taifa hautafikiwa iwapo wananchi watakuwa na afya mbovu, hivyo watahakikisha wanatoa elimu na kusimamia vyema ujenzi wa vyoo bora kwa kila kaya"amesema Dkt,Mwasha,
Kikao hicho kimehudhuria na Katibu Tawala wa Wilaya ya Songwe, ndugu Godfrey Kawacha pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Dkt. Calvin Mwasha ambaye ndiye aliyeiongoza timu ya CHMT katika kikao hicho.




Comments
Post a Comment