Mfumo wa stakabadhi gharani ulivyonufaisha Wakulima wa zao la ufuta mkoani Songwe
MAKALA
Wakulima wapelekwa Morogoro kujifunza mbinu mkoani Morogoro huku wakiibuka na zao la Mbaazi
Na Ibrahim Yassn,
yassin.ibrahimu@yahoo.com 0718382817.
WANANCHI ambao ni wakulima katika halmashauri ya wilaya ya Songwe mkoani Songwe wameeleza jinsi wanavyonufaika na kilimo cha mazao mbalimbali likiwemo zao la ufuta kupitia mfumo stakabadhi gharani,huku mpango uliopo ni kuanza kilimo cha mbaazi.
Asilimia 75 ya wakazi wa Songwe ni wakulima,wafugaji,wavuvi na wachimbaji ambao wanaendesha maisha yao kupitia mazao hayo huku zao la ufuta likiwatajirisha zaidi.
Licha ya wilaya hiyo kuwa ni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu,lakini wakazi wa eneo hilo wameanza kujiingiza katika kilimo huku halmashauri ikiwashika mkono kuwezesha kilimo chenye tija.
Halmashauri hiyo ilianza kuzalisha zao la ufuta kabla ya kuanzishwa kwa wilaya hiyo wakati huo ikiwa chini ya wilaya ya Chunya, ikijulikana kama Tarafa ya Kwimba na Songwe.
Kwa kuwa hawakuwa na stakabadhi gharani, wakulima kwa misimu iliyopita kabla ya mwaka 2022/23 waliuza ufuta kwa soko huria.
Uuzaji wa soko huria uliumiza wakulima kwani wanunuzi walikuwa wakitumia ndoo za plastiki.zenye ujazo wa kilo 20 ambazo wengi wao walidaiwa kuzichemsha na maji ya moto na mchanga ili zitanuke.
Licha ya uwepo wa ulanguzi huo bado uzalishaji zao hilo uliendelea mwaka hadi mwaka na serikaki ikiwaunga mkono kwa kuwapatia pembejeo na kuwahamasisha kujiunga kwenye vikundi.
Hata hivyo msimu wa 2022/23 mfumo wa stakabadhi gharani ulianza rasmi huku zao la ufuta likifanya vizuri zaidi hali iliyopelekea viongozi wa halmahauri hiyo wakiwemo madiwani kwemda kujifunza namna ya kulima zao la mbaazi ili waongeze tija zaidi kwenye kilimo.
Manufaa ya stakabadhi gharani ni gharama za vifungashio kulipwa na mnunuzi, wakulima kuuza mazao kwa bei nzuri kwa njia mnada,wakulima wanapata fedha kwa njia ya mnada, gaharama za usafiri kulipwa na mnunuzi.
Pia faida nyingine ni wakulima kuwa na uhakika wa.mikopo ya Benk, kupata pembejeo kwa njia ya vyama vyao vya ushirika gharama za mtunza ghara hulipwa na mnunuzi.
Kwa upande wa Halmashauri imekuwa ni rahisi kukusanya takwimu sahihi za uzalishaji wa zao hilo na hadi sasa vikundi vimeongezeka kutoka 23 hadi 61.
Kuanzia msimu wa mwaka 2022/23 kwa mfumo wa stakabadhi ghalani mapato ya ufuta yalikuwa Tsh., 792,291,513.80 na msimu wa 2023/24 kwa masoko yote 10 Tsh, 968,899,288.30 zilikusanywa .
Afisa kilimo wilayani Songwe, Ally Kassim Ramadhani anasema katika msimu wa kilimo wa 2021/22 malengo ya uzalishaji yalikuwa tani 9,700 lakini walipata Tani 5,848.800.
Anasema mwaka.2023/23 malengo ni tani 9.700 lakini walizalisha tani 7,556.510 na mwaka 2023/2 4 walikisia kuzalisha tani 12,144.38 lakini walizalisha tani 8,361.797.
"Sababu ya msimu huu kutofikia malengo ni kutokana na mvua kunyesha kupita kiasi lakini wamejipanga msimu huu kugawa mbegu na pembejeo kwa wakulima mapema" anasema ,Ramadhan.
Anaongeza kuwa katazo zaidi la wanunuzi kununua mazao kwa ndoo za kilanguzi ziitwazo Msumbiji badala ya kutumia kilo huku mkulima akipangiwa bei.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Songwe Secilia Kavishe anasema baada serikari ya Rais Dkt, Samia kutoa mafunzo kwa maafisa kilimo na kuwapa vitendea kazi mapat o ya kilimo yamepanda.
Anasema na wao kama halmashauri walilazimika kutoa elimu kwa wakulima pamoja na kuwahamasisha kujiunga kwenye vyama vya ushirika na kufanikiwa kupewa mikopo yenye thamani ya Bilioni 3.4 kutoka benki.
Anasema kupitia mpango huo halmashauri ilipata Tsh, 969,344,965, vyama vya ushirika vilipata Tsh, 585,325,790.wakati wakulima.wa lipata Tsh, 31,365,137,633,huku mikakati ya kuongeza zaidi uzalishaji ikifanyika.
Hata hivyo Kavishe anasema mafanikio hayo yametokana na mipango mizuri kwani Madiwani wa kamati ya mipango na fedha walifanya kstikziara mikoa ya Lindi na Mtwara kujifunza namna ya masoko kupitia mfumo wa 8 of 9œ or 0 ppl9 look lookstakabadhi ghalani .
Anasema baada ya kurejea wilayani humo walizunguka kata zote 18 za walaya ya Songwe kutoa elimu kwa wakulima namna ya kutumia stakabadhi ghalani,ikiwa ni pamoja na kuongeza bajeti ya mbegu zitakazogawiwa bure kwa wakulima.
Anaendelea kusema kuwa katika msimu huu wamejipanga kuongeza kuwango cha utoaji wa mbolea za bure na kuwapa maeneo zaidi ya kulima kwa kuanzia tayari wamewapeleka baadhi ya wakulima Mkoani Morogoro kujifunza zaidi.
Katika kuhakikisha wanayaingiza mazao mengine kwenye mfumo stakabadhi ghalani, madiwani walienda kujifunza klilimo cha mbaazi mkoani wilaya ya Babati na Hanag'i hivyo wanategemea kuwawezesha wakulima kulima mbaazi kuongeza kipato zaidi.
Anasema wakati zoezi hilo linaendelea wameanza kujenga maghara kwenye maeneo muhimu ikiwemo kata ya Kapalala na Manda na tayari wamenunua gari kubwa aina ya Faw kwa ajili ya kubebea mazao ya wakulima kutoka shambani hadi ghalani.
TMX wanatusaidia kupata masoko ya uhakika na sasa vyama vya msingi vya wakulima vimeongezeka kutoa 23 hadi 61 huku idadi ikitarajiwa kuongezeka zaidi" anasema Kavishe.
Mkuu wa wilaya ya Songwe Solomon Itunda anasema wakulima walivyopata fedha nyingi kupitia kilimo cha ufuta hata wilaya imetulia hivyo wamejipanga kuhakikisha wanaharakis hiwa pembejeo mapema ili waongeza tija zaidi ya kilimo.
"Kupia stakabadhi ghalani halmashauri imepata xsudi ya Bilioni 1 na ni chanzo muhimu cha mapato, Mbunge,.Meenyekiti wa halmashauri Mkurugenzi, katibu tawala wamekuwa.wakitoa ushirikiano mkubwa kuwezesha wakulima.kupata mafanikio haya " anasem Dc Itunda.
Anasema kwa sasa.serikali kupitia halmas hauri meongeza fedha zaidi kununua mbegu zitakazogawiwa bure kwa wakulima kilichopo kwa sasa ni kutoa hamasa kwa wakulima kuanA maandaliI mapema.
.Jofrey Shimwinga mkulima na mkazi wa Patamela anasema wamenufaika zaidi kupitia mfumo huo ukilinganisha na awali walipokuwa wakiuza kwenye masoko huru ambapo walanguzi walikuwa wakitumia ndoo kubwa huku wakijipangia bei.
Nae Nathan Samwel mkazi wa Gua anasema licha ya wao kupata kipato katika zao la Tumbaku alijiingiza kwenye kilimo cha ufuta na kujikuta akinufaika zaidi kwani bei iliyopo sokoni ni elekezi na unalipwa kupitia Benki hali iliyoongeza usalama wa fedha zao.
George Lamec mmoja wa viongozi wa kijiji cha Patamela anasema walitii maagizo ya viongozi wao wa halmashauri kwa kuwaita wakulima kuwapa elimu na sasa wamepata manufaa na kwamba hata yeye ni mkulima licha ya kupata mazao mengi amejipanga kulima zaidi msimu ujao likiwemo zao la Mbaazi.
Mzee Isaka Mkalamba mkazi wa Songwe anasema yeye ni kiongozi wa wakulima kupitia ushirika ameona namna wakulima walivyonufaika na kuifanya wilaya kutulia ukilinganisha na ilivyokuwa miaka michache ya nyuma ambapo migogoro ilitokea kutokana na kutopewa elimu.
''Tunamshukuru mkuu wa wilaya,mkurugenzi,Mbunge,mwenyekiti wa halmashauri wakiongozwa na viongozi ngazi ya mkoa ambao hawakulala walifika katika maeneo yetu na kuwapa elimu inayowasaidia kukuza kipato na kuondokana na migogoro''anasema Mkalamba.







Comments
Post a Comment