WACHUNGAJI NA VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KUEPUKA KUWA OMBAOMBA.
Na Abraham Mwaitenda, Songwe
IMEELEZWA kuwa viongozi wa dini wakiwemo wachungaji wa makanisa wametakiwa kufanya kazi za kujiingizia kipato ili kujikwamua kiuchumi kuondokana na uombaomba.
Kauli hiyo imetolewa jana .na mmoja wa wadhamini wa kanisa la Marafiki Duniani Mch.,Erick Roy .raia wa Marekani wakati akizungumza na viongozi wa kanisa la.Friend Church mjini Tunduma.
Mch. Roy amesema kufanya kazi ni Ibada hivyo wachungaji na viongozi wengine wametakiwa kufanya kazi na kuwawezesha waumini wao mbinu za kutafuta mali ili wajikwamue kiuchumi.
Amesema Mungu mwenyewe alifanya kazi siku 6 lakini alipumzika siku ya 7 na akasisitiza kuwa asiyefanya kazi na asile ,hivyo ni wajibu watumishi wa mungu kufanya kazi ili kujiingizia kipato.
Amesema wachungaji wakiwa na uchumi mzuri wataendesha ibada vizuri, waumini wakiwa.na uchumi watahudhuria ibada na kutoa sadaka na fungu la kumi vizuri na kanisa litaemdelea.
" wachungaji wengi wamekuwa wakiendesha maisha kwa kutegemea sadaka za waumini kutokana na uvivu wa kufanya kazi wakijinasibu kuwa watakula vya madhabahuni kitu ambacho si sahihi" amesema.
Amesema Pilisila na Akwila walimjua mungu kabla ya kuonana na Mtume Paulo , Paulo alikuwa akijenga mahema akifanya biashara lakini alitumia mkusanyiko huo kutangaza neno la mungu na watu walimjua na kumtumikia mungu.
Amesema makanisa mengi hayafundishi waumini kuhusu utafutaji wa pesa wamekuwa wakihamasisha utoaji wa sadaka bila kuwafundisha namn a ya kuzitafuta ,Paulo pamoja.na utume wake lakini alitafuta pesa.
"Kuna vifungu vingi vya kuhamasisha utoaji wa sadaka ikiwemo Luka 6 mstali wa 36 inasema toa utabarikiwa , waumini ili waweze kutoa vizuri ni lazima wawezeshwe mbinu za kutafuta hela "amesema.
Nae Mch,Simon.Bumiro Raia wa Kenya amesema suala.la kutoa sadaka na fungu la kumi ni la muh imu na lipo kwenye maandiko ikiwemo Malaki 2 hadi 10 inasema toeni matoleo yote katika hema la mungu mtabarikiwa ili tufanikishe hilo ni lazima tutafute hela.
"Imefikia wakati waumini hawaendi makanisani kisa hawana hela za sadaka, hii si sawa, tuwae limishe waumini mbinu za kutafuta hela , wachungaji tutafute hela, na poa mchungaji hatakiwi kushika hela za sadaka zaidi ya kamati " ame sema, Mch, Bumiro.
Amesema Isaya 52 hadi 58 inasisitiza kujenga kuta zilizobomoka na popote muendako muwe na moyo wa kujenga na kujenga kunataka kipato hivyo amewataka waumini kujiingiza kwenye uzalishaji mali kufanikisha hili.
Mbali na mafundisho hayo pia ilifanyika harambee ya kusaka fedha za ujenzi wa kanisa eneo la Msongwa Tunduma, zaidi ya Milioni 5 zilipatikana.







Comments
Post a Comment