MADIWANI WAPITISHA AZIMIO KUZIITA SHULE MAJINA YA DC NA DED WA SONGWE.

LENGO NI  KUTAMBUA MCHANGO WAO KATIKA KUIMARISHA MAHUSIANO NA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI.

Na Ibrahim Yassin,Songwe. 

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Songwe mkoani hapa,limepitisha azimio la kuzipa majina ya Solomon Itunda (Mkuu wa Wilaya ya Songwe) na CPA. Cecilia Kavishe (Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe) shule mbili mpya ambazo ujenzi wake umeanza.

Lengo la madiwani kupitisha azimio hilo  ni kutambua mchango wa viongozi hao wa kuimarisha ma husiano katika wilaya hiyo pamoja na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.

Azimio hilo limepitishwa jana Jumanne Oktoba 22, 2024 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/20 25 kilichofanyika katika ukumbi wa Sambila uliopo katika ofisi za Halmashauri.



Azimio hilo limepitishwa baada ya madiwani kupata nafasi kila mmoja kujadili sababu za kuzipa shule hizo majina ya viongozi hao, wakieleza kuwa wamekuwa wakiimarisha mahusiano na kusababisha Wilaya kuwa na utulivu.

Mbali na wilaya hiyo kuwa na utulivu Mbunge ,Mwenyekiti wa halmashauri,Mkurugenzi, mkuu wa wilaya, madiwani na viongozi wa CCM kuwa na umoja ,pamoja na kuwa na usimamizi mzuri wa fedha zinazoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.



Katika azimio hilo, Shule ya Amali inayojengwa katika kijiji cha Iseche Kata ya Mwambani ambayo inagharimu Sh1.6 bilioni itaitwa Itunda (Solomon Itunda) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Songwe huku.

Na pia Shule ya sekondari inayojengwa katika Kitongoji cha Kimborokoto Kata ya Mkwajuni itakayogharimu Sh,583 milioni ikipendekezwa kuitwa Cecilia Kavishe ambalo ndilo jina la Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Solomoni Itunda amesema anawashukuru madiwani kwa kutambua mchango wake huku akisisitiza ushirikiano uliotukuka ili wilaya hiyo isonge mara dufu kimaendeleo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo CPA _Cecilia Kavishe (The  Smart Mother) aliliel eza baraza hilo kuwa thamani aliyopewa itaongeza  chachu ya uwajibikaji.

Imekuwa ni kawaida kwa madiwani hao kutoa majina ya viongozi kwenye miradi ambapo Mbunge Philipo Mulugo na mwenyekiti Abraham Sambila yanatumika kwenye shule ikiwa ni pamoja na ukumbi wa halamshauri umepewa jina la Sambi la. 


Ikumbukwe kuwa wilaya ya Songwe ilikuwa haijatulia kutokana na uwepo wa sintofahamu baina ya viongozi kwa viongozi lakini kipindi hiki cha Rais Dkt.Samia kuwaleta Dc Itunda na Ded Kavishe wilaya imetulia na inasonga mbele kimaendeleo. 


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa