UONGOZI WA JUU BONDE LA MTO SONGWE WATOLEA UFAFANUZI MIKAKATI ILIYOPO KUDHIBITI KUHAMA HAMA KWA MPAKA TANZANIA NA MALAWI.





Na Ibrahim Yassin,yassin.ibrahimu@yahoo.com  0718382817

Imeelezwa kuwa uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi hadi kwenye kingo za mto imetajwa kuwa chanzo mto Songwe kugawa upya mpaka wa Tanzania na Malawi.

DiraKamilifu ilifika kijijini humo kuzungumza na wananchi wakiwemo viongozi wa pande zote mbili kujua sababu ya uharibifu huo na mipango iliyopo ya kunusuru hali hiyo.

Umoja wa waendesha mitumbwi wanaovusha watu na mizigo kwenda upande wa pili wa nchi ,wakiongozwa na mjumbe wa kijiji cha Mpung uti,Ambele Mwaikeneke,anasema uharibifu wa mazingira hasa watu kulima hadi kwenye kingo za mito ndiyo sababu kubwa,

Nae Harodi Mwakatundu mwenyekiti wa CCM kata ya Katumba Songwe alilieleza gazeti hili kuwa wakazi wa pande zote mbili wamekuwa wakiharibu mazingira kwa kulima na kufanya shughuri za kibinadamu hadi kwenye kingo za mto huo.

Hata hivyo anasema wanafanya kila linalowezekana kuongeza katazo na kudhibiti uharibifu huo ili kurejesha njia ya asili ya mto huo jambo ambalo linahitaji  ushirikiano na nguvu ya ziada.


Kwa upande wake Chief Mwakabhoko kiongozi mkuu anayeongoza ukanda huo upande wa Malawi anasema mto huo unaweza kuanzisha mpaka mwingine hali itakayoweza kuathiri nchi hizo endapo hatua za makusudi za udhibiti hazitochukuliwa.

Mbunge wa jimbo la Kyela Ally Mlagila Jumbe anasema ni kweli hali ya uharibifu wa mazingira ni mkubwa,hivyo kuna mikakati imewekwa na pande zote mbili kuyavuna maji ya mto huo ili kuyaelekeza kwenye mashamba ambapo kwa Tanzania zipo ekari zaidi ya 35,000 na Malawi ekari 350.

Mkuu wa wilaya hiyo,Josephine Manase licha ya kukiri uwepo wa hali hiyo anasema wapo kwenye mikakati endelevu na ya kudumu ya kumaliza tatizo hilo na pia alizungumza na wananchi wanaandaa mifuko ya sandarusi ili waweke vitu vizito na kuweka kwenye maeneo yaliyoathiriwa zaidi.

Moses Nkhunkuyu msemaji wa wizara ya mawasiliano wa Malawi,anasema yeye hajapata taarifa yeyote hivyo aliomba chombo hiki cha habari kimpe taarifa zilizopo ili na yeye apeleke kwenye serikali ya nchini Malawi ili ifanyiwe kazi.

KATIBU MTENDAJI BONDE HILO AELEZA MIKAKATI YA UDHIBITI..

Akizungumza na Dirakamilifu Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe, Dkt. Ladislaus Kyaruzi Leonidas, anasema kuwa mto huo unakabiliwa na changamoto kad haa, ikiwemo uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.



Dkt. Kyaruzi anaeleza kuwa ukataji wa miti na kufyeka magugu kwenye kingo za mto unachangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa udongo hali inayosababisha mto kubadilisha mkon do na kuunda mpaka mpya kati ya nchi hizo mbili.

“Nikweli mto una changamoto ya kuhama-hama, na hali hii haijaanza leo, bali imekuwepo kwa muda mrefu. Hata hivyo, tunafanya jitihada za kuweka mazingira bora ili kukabiliana na changamoto hizi,” anasema Dkt. Kyaruzi.

Anasema kuwa mojawapo ya mikakati iliyowekwa ili kupunguza presha ya wananchi kuharibu mazingira ni kuwawezesha kwa kuwapatia mifugo kama Ng’ombe, Mbuzi, pamoja na kufadhili miradi ya ufugaji wa Nyuki na ujenzi wa mabwawa ya Samaki. 

Miradi hii inawapatia wananchi kipato mbadala na kuwafanya wawe walinzi wa mazingira.

Anaongeza kuwa miradi ya ufugaji wa nyuki, ambapo mizinga imewekwa kwenye mapori, imechangia kwa kiasi kikubwa utunzaji wa mazingira kwani wananchi wanatunza mapori hayo. 

Anaongeza kuwa Miradi hii imekuwa ikifanyika katika wilaya za Chitipa na Karonga nchini Malawi, na wilaya za Kyela, Ileje, Momba, Mbeya Vijijini, na Mbozi nchini Tanzania.

Dkt. Kyaruzi alieleza kuwa miradi hii inafadhiliwa na Global Environment Facility (GEF) kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

 Tayari wananchi wameanza kunufaika na mifugo pamoja na elimu juu ya utunzaji wa mazingira na upandaji miti ili kuboresha hali ya mazingira.


Kuhusu mradi mkubwa wa ujenzi wa bwawa lenye uwezo wa kuzalisha umeme wa mega wati 180, Dkt. Kyaruzi alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani milio ni 851.1, na zaidi ya watu 450,000 watan ufaika. 

Anaongeza kuwa serikali za Tanzania na Malawi ziko katika hatua ya kutafuta wawekezaji kwa ajili ya mradi hiyo.

Dkt. Kyaruzi alieleza kuwa wananchi wanaoishi kandokando ya Mto Songwe walielimishwa kuacha kufanya kilimo ndani ya mita 60 kutoka kingo za mto, kama ilivyokubaliwa na pande zote mbili, tofauti na madai ya wananchi kuhusu mita 15.

Alifafanua kuwa mita 15 za kwanza kutoka kingo za mto zimetengwa kwa upandaji wa miti ya matunda kama Miembe, Mawese, Machungwa, na kokoa ili kusaidia kupunguza mmomonyoko wa udongo.

 Mita 15 zinazofuata inaweza kupandwa miti ya mbao, huku mita 30 zilizobaki zikifaa kwa kilimo cha mazao yanayosaidia kuimarisha udongo, kama vile Mihogo, Mahindi, na mazao mengine, badala ya mazao yanayosababisha mmomonyoko kama Mpunga.



''Hadi sasa tumezalisha miche mingi ambayo tutaigawa kwa wananchi wapande pembezoni mwa mto,pia tumewapa miradi ikiwemo ng'ombe wa maziwa ili wapate kujikwamua kiuchumi huku wakiwa ni walinzi wakuu wa maeneo hayo'anasema Dkt,Kyaruzi.

Pia alisisitiza kuwa elimu kwa wananchi inaendelea kutolewa ili kuhakikisha mradi huu unaleta manufaa kwa mataifa yote mawili kwa kupunguza kasi ya uharibifu wa mazingira, huku akiongeza kuwa miradi mikubwa inayotarajia kukamilika itasaidia kudhibiti kasi ya maji na kupunguza mto kuhama-hama.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa