Mama Samia na Wafanyabiashara Songwe wampa 5 Mbunge Fiyao kwa namna anavyoshughulika na kero za Wananchi



Na Ibrahim Yassin.Songwe

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu amepongeza mbunge wa viti maa lum mkoani humo Stella Fiyao kwa kutekeleza ma jukumu yake pamoja na kutambua kazi zilizofaan ywa na serikali.

Dkt, Samia aliyasema hayo jana wakati akiwas alimia wananchi wa mkoa wa Songwe eneo la Tunduma akitokea mikoa ya Katavi na Rukwa alikokuwa kwenye ziara ya kikazi.

Alisema Mbunge Fiyao wa Chadema ametambua kazi zilizofanywa na serikali ni jambo zuri na kwak utambua umuhimu wa demokrasia walifanya meri dhiano na vyama vyote na sasa wanafanya kazi kwa kushirikiana.



Awali akizungumza baada ya kupanda kukwaani mbunge Fiyao alisema anaipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt,Sam ia.kwa kwa kuleta maendekeo kwani Tanzania kwa sasa inang'ara.

Alisema kwa upande wa vyama vya upinzani wamekuwa wakinena rugha moja wanakula na kukaa.pamoja ukilinganiaha na miaka ya nyuma ambapo waliishi kwa chuki.

Fiyao alitumia jukwaa hilo kumueleza Rais Samia kupitia hadahara hiyo kuwaondolea wafanyabi ashara changamoto zao kwani asilimia.kubwa wamekimbilia upande wa Zambia.

"Mh Rais nashukuru kwa ujio wake naomba ziang alie changamoto za wafanyabiashara na uzitatue ili warejee kwani maduka yote makubwa yaliopo Nakonde Zambia ni ya watanzania, mapato mengi yanapotea" alisema Fiyao.

Kupitia kauli hiyo mfanyabiashara mtanzania Zuberi Issa anayemiliki duka upande wa Zambia alisema mbunge Fiyao ni mtu na nusu amewase mea changamoto na iwapo watawekewa mazingi ra rafiki watarejea.



Akizungumzia hali ya biashara kupitia mkutano huo waziri wa viwanda Dkt, Suleiman Jafo alise ma watafanya kila liwezekanalo kuweka mazing ira rafiki kwa wafanyabiashara

Baada ya kauli za viongozi hao Rais Dkt, Samia alisema changamoto zitatatuliwa na kusisitiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.

Sambamba na hilo Dkt Samia alimuagiza waziri wa afya Ommy Mwalimu kuhakikisha wanamnun ulia mguu wa banda mtoto mlemavu aliyejitokeza kwenye mkutano huo.

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa