Mbunge Fiyao adhamiria kukuza vipaji vya katika michezo kwa kuanzisha ligi
Na Ibrahim Yassin.Songwe
LIGI ya mchezo wa mpira wa miguu mkoani Songwe kwa ajili ya kutafuta na kuibua vipaji inatarajia kuanza siku za hivi karibuni wilayani Ileje na kumalizika Halmashauri ya mji Tunduma.
Mchezo huo pendwa wa mpira wa miguu Duniani umedhaminiwa na Mbunge viti Maalum mkoa wa Songwe Stella fiyao huku akitenga kitita cha fedha kwa ajili ya zawadi.
Akizungumza leo Julai 26/2024 mbunge Stella Fiyao (CHADEMA) amesema lengo la kuanzisha ligi hiyo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt, Samia katika sekta ya michezo.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa mchezo huo jinsi unavyotoa ajira Rais Dkt.Samia ameongeza bajeti ili kufanikisha na kuukuza maradufu mchezo huo pamoja na michezo mingine.
"Rais Dkt Samia katika utawala wake mpira wa miguu kwa wanaume na wanawake umekuwa na Nchi imetangazika hivyo namuunga mkono kwa kuanzisha ligi kukuza vipaji vya vijana"amesema Fiyao.
Hata hivyo Fiyao amewasihi wazazi kutowakataza watoto zao hasa wa kike kucheza mpira wa miguu akisema mpira ni ajira kwani hivi juzi tu wasichana wawili wamesajiliwa ligi kuu ya Uingereza hivyo aliwataka wawape sapoti watoto zao kwenye mchezo wa mpira wa miguu^ amesema.
Amesema mwaka jana alianzisha ligi ya Mpira wa miguu mkoani humo ikichezwa halmashauri ya mji Tunduma ambapo mshindi wa kwanza alipata Tsh, 1,000,000,Mshindi wa 2 TSh 500,000.
Ameongeza kuwa Mshindi wa 3 TSh 300,000, Timu yenye nidhamu ilipata Tsh, 100,000,huku Jezi set 1 na mpira 1zilitolewa kwa kila team shiriki
Mbunge fiyao amesema ligi hii inatarajia kufanyika wilayani Ileje na itafanyika tena Tunduma na mfumo wa zawadi ni hivyo hivyo,huku akiwasihi vijana kushiriki.
"Kwa kuwa mpira ni ajira nawasihi vijana wasikae vijiweni waanze mazoezi waingie kwenye ushiriki ili wapatikane vijana watakaoweza kusajiliwa kwenye virabu vikubwa hali itakayowaondoa kwenye lindi la umasikini^amesema Fiyao.



Comments
Post a Comment