RC-TUMIENI FURSA YA MRADI WA UMWAGILIAJI KUJIINUA KIUCHUMI




Na Israel Mwaisaka, Nkasi

Mkuu wa mkoa Rukwa Charles Makongoro Nyerere amewataka Wananchi wa kata za Kipili, Kirando na Itete wilayani Nkasi kutumia fursa ya mradi wa umwagiliaji unaojengwa katika kata hizo kuinua kipato Chao Huku akiwataka Wananchi kulinda miundombinu ya mradi huo Ili use na manufaa Kwa jamii kama ilivyokusudiwa na serikali.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo Jana wakati akishuhudia utiaji Saini na makabidhiano ya mradi wa skimu ya umwagiliaji Lwafi-Katongolo kati ya tume ya taifa ya taifa ya umwagiliaji na mkandarasi M/S Halem Construction Company Limited
Alisema licha ya serikali kutumia fedha nyingi kukamilisha mradi huo hautakuwa na maana kama watashindwa kuutunza na kuulinda na kuwa lengo la serikali ni kutaka kuona uzalishaji unapanda na Wakulima kuweza kulima kilimo Cha kibiashara na kujikwanua kiuchumi na kubwa ni kutaka kuona jamii inabadilika Kwa kuwa na maisha bora.

Akitoa taarifa ya mradi huo Mhandisi Lucas Mganda ambaye pia ndiye msimamizi mkuu wa mradi huo wa umwagiliaji wa mkoa alidai kuwa mradi huo utagharimu Bilioni 20.9 na utakelekelezwa Kwa siku 720 sawa na miezi 24 ambao utakamilika Julai 25,2026.

Alisema kuwa mradi huo ukikamilika utawanufaisha wakazi 30,000 wa kata hizo tatu na kuwezesha kumwagilia hekta 33,000 na kuongeza kiwango Cha uzalishaji Hadi kufikia gunia 50 Hadi 75 Kwa hekta Moja .

Makamo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Stephen Kayogolo alidai kuwa Moja kati ya miradi iliyokuwa ikijadiliwa Kwa upana katika vikao mbalimbali vya halmashauri ni pamoja na mradi huo licha ya serikali ilikua ikiendelea kutoa fedha Kila wakati lakini zilikua hazikidhi ukamilishaji wa mradi huo Kwa asilimia 100 .


Alidai kuwa kitendo Cha serikali kutoa Bilioni 20.9 kilikua hakitarajiwi lakini sasa fedha hizo zimetolewa na kuwa ndogo Yao ya kuwa na skimu kubwa ya umwagiliaji katika wilaya ya Nkasi na mkoa Kwa ujumla imefikiwa na kubwa ni Wananchi kujipanga vyema katika kuhakikisha kuwa mradi huo wanaotumia ipasavyo katika kujiletea maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kasikazini Aida Khenan Kwa upande wake alisema kuwa yeye kama mbunge ameupigania mradi huo ambapo amekua akiishawishi wizara ya kilimo kuachana na kutoa fedha ndogo ndogo na kuishauri kutoa fedha ambayo itakamilisha mradi huo Kwa ujumla na kuwa Kwa kufanya hivyo kutawezesha kuonekana Kwa matokeo ya chanya ya mradi huo.

Hivyo aliwataka viongozi kutoingiza masuala ya kisiasa wakati wa utekelezaji wa mradi huo na kuwaacha Wataalamu wautekeleze mradi huo kiutaalamu na kuwa maamuzi ya kisiasa yakiingizwa kwenye utekelezaji wa mradi huo watafika sehemu watakwama na kuuharibu mradi ambao unategemewa Kwa kiasi kikubwa na Wananchi wa kata hizo tatu za mwambao wa ziwa Tanganyika.


Awali mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nkasi Aljabri Ali Sudi alimweleza mkuu wa mkoa kuwa wao kama Chama wataendelea kuisumbua serikali kuhakikisha kwamba mradi huo inatekelezeka sawa na mkataba waliotiliana na kuwataka Wananchi kuwa walinzi wa mradi huo Kwa kuhakikisha vifaa vyote vya ujenzi haviibiwi na watekelezaji wa mradi huo na wao kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa Kwa viongozi wa serikali pale wanapoona vifaa vya ujenzi wa mradi huo vinauzwa mitaani Kwa bei ndogo na wao kuikataa hari hiyo Ili kuweza kulifikia lengo halisi la ukamilishaji wa mradi huo.

Kwa upande wao Wananchi wa tarafa ya Kirando wamempongeza Mhe,Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza kilio Chao na kuweza kutoa fedha hizo ambazo zinakwenda kuwa Mkombozi kwao na kuahidi wao kuwa Watu wa kwanza katika kuulinda mradi huo na kuhakikisha unakamilika ipasavyo.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa