SIKU 7 ZA RAIS DKT,SAMIA ZILIVYOACHA HISTORIA NA ALAMA MIKOA YA KATAVI ,RUKWA NA SONGWE

                     MAKALA

AZINDUA MIRADI MIKUBWA NA YA KIMKAKATI KATAVI NA RUKWA WANANCHI HAWAKUTAKA AONDOKE.

Na Ibrahim Yassin,Songwe

Zimekua siku 7 za moto zenye kishindo cha maendeleo toka Julai 12 hadi wiki hii Jumatano Julai 87, 2024 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muunga no wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alikua na ziara kubwa na ya kimkakati kwenye mikoa miwili ya Nyanda za Juu Kusini.
Takribani siku 6 alizokuwepo kwenye mikoa hii ya pembezoni mwa nchi yetu zimetuma ujumbe kwa kila Mtanzania jinsi kazi kubwa ya maendeleo inavyozidi kufanyika kila kona ya Taifa Rais Dkt,Samia alipokuwa na timu yake mikoa ya Katavi na Rukwa kasha akapita mkoa wa Songwe siku ya 7. 

Miaka ya nyuma kulikua na msemo kuwa mikoa ya pembezoni mwa nchi yetu ilikua kama ni mikoa iliyoachwa nyuma kimaendeleo, lakini leo miaka mitatu ya Rais Samia madarakani imefuta misemo hiyo kwa kuangalia jinsi miradi mikubwa ya kutoa huduma kwa wananchi ilivyotekelezwa kwenye mikoa hiyo huku Rais Samia akiizundua.

Katika ziara hii, Rais Samia amefanya shughuli mbalimbali za maendeleo na za kijamii ambapo ukiacha kazi kubwa ya kusukuma maendeleo, alish iriki kufunga Wiki ya Wazazi iliyofanyika Julai 13, 2024 hapo Katavi kwe nye viwanja vya Azimio,Baada ya hapo ikawa mfululizo wa shughuli za maendeleo na uzinduzi wa miradi mikubwa.



Mkoa wa Katavi pekee umevunja rekodi ya kupata fedha nyingi za maend eleo toka Tanzania ianzishwe. mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mri ndoko anasema mkoa huo haujawahi kupata fedha nyingi za maendeleo kama inavyopata sasa chini ya Rais Samia ambapo ndani ya miaka mitatu Katavi imepokea Trilioni 1 na Bilioni 246 na milioni 776 za maendeleo ambazo zimefanya mapinduzi makubwa ya maendeleo. 

Mikoa hii ni ya kilimo na zao kuu ni mahindi na tayali akiwa kwenye mkoa wa Katavi, Rais Dkt,Samia alipandisha bei ya mahindi ya wakulima kwa kilo kutoka Tsh 500 kwa kilo hadi 600 maeneo ya vijijini na 650 mijini.

Alipofika mkoani Rukwa tarehe 17 Julai 2024 akihitimisha ziara yake kwenye uwanja wa Nelson Mandela pale Sumbawanga mjini aliongeza tena bei ya mahindi hadi 700 kutoka ile ya awali ya Tshs 500 tu.




Katika harakati za kuufungua zaidi mkoa wa Katavi ambao kwasasa unakua kwa kasi kubwa hasa kwa utalii kwenye Mbuga ya Katavi, Bandari ya Kale ma na ukuaji wa center yake ya Mpa nda, Serikali ya Rais Samia imefanya maboresho ya uwanja wa ndege wa Mpanda na kwenye ziara hii mkoani Katavi Rais Samia alikagua ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege huo uliogharimu Bilioni 1.4.

Mkoa wa Katavi toka toka Tanzania ipate uhurui haujawahi kupata umeme wa Grid ya Taifa na mkoa hutumia zaidi ya Bilioni 2 kila mwezi kuwasha majenereta kwa umeme. Serikali ya Rais Samia imetumia Bilioni 48 kujenga Kituo kikubwa cha kupoza umeme katika Grid ya Taifa pale Inyonga Mpanda ambacho kitaufungua mkoa wa Katavi kwa kuwa na umeme wa uhakika baada ya muda mrefu kuukosa.



Kwa jinsi Katavi inavyokua kwa kasi, ulinzi na usalama wake ni muhimu zaidi ili kuchochea shughuli za kiuchumi na hapo Rais Samia akazindua Jengo la kisasa la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi na kuamsha shangwe kwa wananchi.

Kwasababu Katavi ni mkoa wa kilimo unaolisha Taifa, kwenye ziara hii pia Rais Samia alizind ua maghala na vihenge vya kisasa vya kuhifadhia nafaka vya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Ofisi ya Wataalamu wa NFRA.

Pia alizindua Ghala na vihenge vyote jumla vinaweza kuhifadhi Tani zaidi ya Elfu 25 kwa mpigo. Hapo alizindua pia vipimo vya kisasa vya kupima mazao ya wakulima na sasa chini ya Rais Samia hakuna tena mkulima kuibiwa mazao yake


Kwasababu Katavi ni mkoa wa kilimo unaolisha Taifa, kwenye ziara hii pia Rais Samia alizind ua maghala na vihenge vya kisasa vya kuhifadhia nafaka vya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Ofisi ya Wataalamu wa NFRA.

Pia alizindua Ghala na vihenge vyote jumla vinaweza kuhifadhi Tani zaidi ya Elfu 25 kwa mpigo. Hapo alizindua pia vipimo vya kisasa vya kupima mazao ya wakulima na sasa chini ya Rais Samia hakuna tena mkulima kuibiwa mazao yake.

Samia alizind ua maghala na vihenge vya kisasa vya kuhifadhia nafaka vya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Ofisi ya Wataalamu wa NFRA.

Pia alizindua Ghala na vihenge vyote jumla vinaweza kuhifadhi Tani zaidi ya Elfu 25 kwa mpigo. Hapo alizindua pia vipimo vya kisasa vya kupima mazao ya wakulima na sasa chini ya Rais Samia hakuna tena mkulima kuibiwa mazao yake.



Hapa Katavi Rais Samia alitembelea kuona kazi kubwa ya serikali yake ya kujenga hospitali kubwa ya rufaa ya mkoa wa Katavi ambayo imeshaanza kutoa huduma na hakuna tena usumbufu wa wananchi

kutafuta huduma kubwa za matibabu mbali, badala yake zipo mikoani hukohuko kwao.

AKIWA MKOANI RUKWA.

Akiwa mkoani Rukwa Rais Dkt,Samia alizindua mfululizo wa miradi ya maendeleo huku mkoa huo ukipata fedha nyingi za maendeleo ambazo hazijawahi kupata toka mkoa na Tanzania ianze. Hapa akikagua na kuzindua hospitali kubwa na ya kisasa ya wilaya ya Nkasi ambayo zaidi ya Bilioni 3 zimejenga ili kutoa huduma zote kwa wananchi wa Nkasi.

Katika kufikisha huduma karibu na wananchi wa Rukwa waliokua wanasafiri hadi Sumbawanga mjini takribani Km zaidi ya 100 kufuata huduma za utawala, serikali ya Rais Samia ikatoa Bilioni 4.5 kujenga majengo ya kisasa ya halmashauri ya wilaya ya Kalambo pale kwenye mji wa Matai ili wananchi wapate huduma hapohapo na si kusafiri mbali kwenda Sumbawanga. hii ni dhamira ya Rais Samia kufikisha huduma karibu na wananchi.

Kama nilivyoandika mwanzo, mikoa hii ya pembezoni mwa nchi hasa Rukwa zamani ilihisiwa kusahaulika, sasa Rais Samia ameondoa hiyo dhana kwa kuifungua kiuchumi mikoa hii kwa miundombinu, huduma za jamii na kila kitu na ndiyo maana kwenye ziara hii Rais Samia alizin dua barabara kubwa ya uchumi inayokupeleka mpaka Bandari ya Kasanga kuelekea nchini Zam bia, barabara ya Sumbawanga- Matai- Kasanga inayounganisha hadi Bandari ya Kasanga yenye Km 107 iliyojengwa kwa Bilioni 150.

Tayali Rais Samia alizindua barabara hii inayokwenda kufungua uchumi wa Rukwa kufungamanisha na bandari na nchi ya Zambia. 

Rukwa ni mkoa wa kilimo cha mahindi ndio zao kubwa la biashara. Kwenye ziara hii baada ya kuzindua hospitali, huduma za utawala na barabara, Rais Samia alizindua pia maghala na vihen ge vikubwa vya kuhifadhia nafaka na mazao kwenye mkoa huu wa Rukwa unaolisha Taifa letu. Maghala na vihenge hivi vya Bilioni 14 pale kijiji cha Kanondo- Sumbawanga alizindua Rais Samia ili kuongeza uwezo zaidi wa Taifa kuhifadhi mazao kwa mauzo nje na matumizi wakati wa dharula

Kila aina ya huduma Rais Samia anafikisha kwenye mikoa hii ya pembezoni mwa nchi ili kuifungua zaidi na kuvunja kabisa ile dhana kwamba ilisahaulika. Kwenye ziara yake hii Rais Samia alizindua Chuo cha VETA kilichotumia Bilioni 6.08 kilichopo Kashai Sumbawanga mjini ili kupika vijana zaidi.

Tayali Chuo hiki cha VETA Sumbawanga Rais Samia amekizindua na kimeanza kutoa huduma ya kupika vijana kwa fani za ujuzi.Rais Dkt, Samia ameamua kuufungua zaidi mkoa wa Rukwa na ndiyo maana kwenye ziara hii pamoja na shughuli zingine kubwa aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa ndege wa Rukwa uliofika asilimia 18. 


Hapa Rukwa akazindua pia Chuo cha Ualimu Sumbawanga,akawe ka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Rukwa iliyopo kijiji cha Mtin dilo pale Laela.

Na sasa Rukwa Chuo Kikuu ni kawaida ambapo Rais Samia aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kampusi ya Rukwa ili kupika Wataalamu zaidi. Tukumbuke Rukwa walilia muda mrefu kutokua na Chuo Kikuu.

 Hapa Sumbawanga pia aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Km 6 kwenda Kaengesa Seminary.
 

Hakuna ubishi na kila Mtanzania ameona kwamba, siku 6 alizofanya ziara kwenye mikoa hii miwili ya Katavi na Rukwa imedhihirisha kazi kubwa iliyofanyika kwa miaka yake mitatu ya uongozi wake huku akifuta kabisa dhana kwamba mikoa hii ya pembezoni imeachwa nyuma. Huyu ndiyo Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mama wa Kazi na Vitendo tu.

AKIWA MKOA WA SONGWE.

Akiwa katika eneo la Transfoma halmashauri ya mji Tunduma,Rais Dkt,Samia aliwasalimia wananchi ambapo mkuu wa mkoa,wabunge na viongozi wa chama walipata nafasi ya kusema jambo kwani penye ugeni mkubwa lazima useme jambo ili uweze kusaidiwa.

Kabla ya Rais kusema jambo Mbunge wa jimbo la Tunduma David Silinde alieleza jinsi Tundum a ilivyopaa kiuchumi na hata kujengwa miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta zote huku akisifu uongozi wa Rais Samia ndani ya miaka 3 ulivyojenga miradi inayogusa jamii.

Nae Mbunge viti maalum mkoani Songwe Stella Fiyao (CHADEMA) hakusita kuisifu serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt,Samia kwa jinsi ilivyojenga miradi mikubwa na midogo huku akisema mama amewaunganisha na kuwa kitu kimoja licha ya kuwa Tunduma miaka ya nyuma waliishi kwa visa kati ya chadema na ccm.

Mbali na hilo Fiyao alitumia nafasi hii kumuomba Rais Samia kuweka mazingira Rafiki ya wafanyabiashara akisema asilimia 75 ya maduka makubwa yaliyopo upande wa Nakonde nchini Zambia yanamilikiwa na Watanania ambao huenda walikimbilia huko kutokana na utitili wa kodi miaka ya nyuma.

Nae George Mwenisongole Mbunge wa Mbozi na Japhet Hasunga Mbunge wa Vwawa mkoani Songwe kwa nyakati tofauti baada ya kupewa nafasi ya kusema hawakusita kusifu kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya sita huku Mbunge Hasunga akikazia ombi la mji wa Vwawa kupewa manispaa.

Juliana Shonza na Neema Mwandabila wabunge viti maalum (CCM) mkoani humo,walisema kwa kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia wananchi wamemuahidi kumpa kura za ndiyo 2025 kwani mambo mengi yaliyokwama miaka ya nyuma katika utawala wa mama yamefanyiwa kazi.

Mbunge wa jimbo Songwe Philipo Mulugo kwa upande wake alisifu utawala wa Rais Dkt,Samia akisema anatembea kifua mbele baada ya kero zote kubwa ndani ya jimbo lake kutatuliwa ikiwe mo suala la stakabadhi gharani na wachimbaji wadogo ambao kwa sasa wanafanya kazi vizuri baada ya kutekelezewa madai yao.

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo kwa upande wake anasema Rais Dkt,Samia amefanya kazi kubwa ya kuwaunganisha wananchi kuwa wamoja bila kujali itikadi za vyama vyao,dini na kabila kwani wamekuwa wakinena rugha moja na kushirikiana katika shughuri za maendeleo. 

Ifahamike kuwa mambo yote ya kimaendeleo yaliyofanywa katika utawala wa Rais Dkt,Samia ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ambapo katiba ya chama na ilani zake zinaeleza utatuzi wa miradi katika sekta zote na hilo limefanyika.

Baada ya viongozi wa mkoa wa Songwe kueleza jinsi Rais Dkt,Samia alivyofanya mambo makubwa mkoani humo,Rais Samia akiwa juu ya gari alimuona kijana mlemavu mwenye mguu mmoja ambap o alimwita na kumuagiza waziri wa afya Ummy Mwalimu kuhakikisha anamnunulia mguu wa bandia kwa fedha za ofisi yake.

 

Mwisho….Mwandishi wa makala haya ni Ibrahim Yassin,anaopatikana kwa simu namba 0718382817-0766936392 barua pepe…yassin.ibrahimu@yahoo.com

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa