Mbunge Fiyao atoa msaada wa Mil 3 kwa Wagonjwa na Wafungwa huku Wananchi wakitoa pongezi
Na.Ibrahim Yassin Songwe
WANANCHI wa wilaya zilizopo mkoani Songwe wamempongeza mbunge viti maalum mkoani humo Stella Fiyao (CHADEMA) kwa kutoa misaada ya mashuka,madishi,mchele,Maharage na taulo za kike kwa wafungwa na wagonjwa vikiwa na thamani ya Tsh Milioni zaidi ya Milion 3.
Wakizungumza.leo Julai 19 /2024.wananchi hao wamesema kwa kitendo alichokifanya Mbunge huuo kwa kutoa misaada hiyo Mungu atampa maisha marefu kwani kitendo cha wafungwa magerezani na wagonjwa hospitalini kupewa mahitaji wanapata faraja.
Samweli Mtafya mkazi wa Ileje amesema alipo ona mbunge huyo amefika wilaya ya Ileje kutoa misaada hiyo kwa wagonjwa alifurahi na kusema huo ni mfano wa kuigwa kwa wadau wengine kuona umuhimu wa kusaidia wenye uhitaji.
Sarafina Nashihuya mkazi wa Ileje amesema wana kila sababu ya kumpongeza Mbunge Fiyao kwa kuona wafungwa na wagonjwa wanahitaji mahitaji muhimu hivyo amefanya jambo jema kuwapa misaada wenye uhitaji.
Kwa upande wake Mbunge Stella Fiyao amesem a.yeye kama kiongozi wa wananchi kwa.kutam bua umuhimu wa wafungwa na wagonjwa ame amua kutoa Milioni zaidi ya Milioni 3 kununua mahitaji hayo na kuwagawia ili kupunguza makali ya mahitaji yao.
Amesema ametoa mashuka na madishi pamoja na taulo za kike hispitali ya wilaya,kwa upande wa Zahanati yanmagereza ametoa mashuka,mchele ,Maharage,madishi na taulo za kile kwa.wafungw a wanawake.
Mbunge Fiyao ameongeza kuwa katika kituo cha afya Itale wilayani Ileje ameroa mashuka na madishi vifaa hivyo kwa ujumla wake vina thamani ya Ths Milioni 3.3.
Amesema baada ya kutoa misaada hiyo anataraj ia kufanya ziara kila wilaya kuona changamoto zin azowakumba wananchi ikiwa.ni pamoja na kuba dilishana nao mawazo ili anapoenda bungeni awe na yakuzungumza.
"Lengo la ziara ni kukusanya changamoto wan azo kutana nazo wananchi wa wilaya ya Ileje,Son gweNanyaro,Mbozi na Momba katika hospital, vituo vya Afya na magereza pamoja na kukusanya changamoto na kueza kuzitatua "amesema.




Comments
Post a Comment