TRA Songwe yawapiga tafu Polisi kwa kuwapatia gari ili kusaidia shughuli za kijeshi



Na.Ibrahim Yassin Songwe

Afisa Mnadhimu namba 02 wa Polisi Mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Geofrey Munguajuna amepokea gari hilo kutoka mamlaka ya mapato kusaidia shughuri za kijeshi.

Afisa huyo akiambatana na Msimamizi wa Magari ya Polisi Mkoa wa Songwe Mkaguzi wa Polisi Kas ibert Kapondo wamepokea Gari aina ya Toyota Mark X lililotumika kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kusaidia shughuli za Jeshi la Polisi.

Gari hilo limetolewa leo Julai 25, 2024 na Zahor Mohammed Salum ambaye ni Meneja Msaidizi wa Forodha Mkoa wa Songwe kwa ajili ya kusaidia kazi za kila siku za Jeshi la Polisi.



SSP Munguajuna ameishukuru Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Songwe kwa msaada walioutoa na amewaomba kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika harakati za kuzuia na kupambana na uhalifu na wahalifu ili jamii iendelee kuwa salama kwa manufaa na maendeleo ya nchi yetu.7.

Jeshi la polisi mkoani hapa limekuwa likifanya kazi kwa ushirikiano na maafisa wa mamlaka hiyo hivyo zawadi hiyo ni kuimarisha mahusiano zaidi katika utendaji kazi.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa