Watendaji wa jeshi la Polisi Songwe wapewa mafunzo ya kisayansi



Na IbrahimYassin.Songwe

Kamishina wa uchaguzi wa kisayansi CP Shabani Hiki ameendesha mafunzo ya uchaguzi wa Kisayansi kwa watendaji wa jeshi la polisi mkoani Songw e.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Julai 19 mwaka huu katika ukumbi wa jeshi hilo mkoani hapa huku maafisa mbalimbali wa jeshi hilo wakiudhuria mafunzo hayo.



Waliohudhuria pia katika mafunzo hayo ni watendaji wa taasisi mbalimbali zinazofanya kazi na jeshi la polisi ambao ni madaktari,wanasheria , na ofisi ya Taifa ya mashitaka mkoa wa Songwe.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Polisi uliopo Vwawa Mbozi yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo katika upelelezi wa matukio ya jinai, na ukusanyaji wa ushahidi na vielelezo kwa kutumia uchunguzi wa Kisayansi.


Kwa mujibu wa afisa habari wa jeshi hilo mkoani hapa Issa Mwandagala ni kuwa uongozi unaoendesha mafunzo hayo ni watazungumza na vyombo vya habari pindi mafunzo yatakapofikia tamati.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa