Shonza awaasa Watumishi wa idara ya afya kuwa na lugha za staa kwa Wagonjwa
Na Ibrahim Yassin.Songwe.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Songwe Juliana Shonza (CCM) ametoa wito kwa watumishi idara ya afya mkoani Songwe kuwa na lugha za staa kwa wagonjwa.
Shonza aliyasema hayo jana wakati akigawa zawadi kwa akina mama wajawazito na watoto katika hospitali ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe pamoja na kukagua ujenzi wa jengo la mama na mtoto lililotolewa Milioni 900.
Alisema siku za nyuma akiwa na uongozi wa chama alifika hospitalini hapo na kukuta malalamiko mengi ikiwemo lugha za matusi kwa wajaw azito wanaofika hapo kujifungua.
Alisema mgonjwa anahitaji faraja ili aweze kujifungua salama na hilo alilifikisha kwa waziri wa afy a Ummy Mwalimu hali iliyohamisha watumishi katika hospitali hiyo.
" Nawaomba tuwe na lugha za staa kwa akina mama hawa, na ni marufuku pia kuwatoza fedha akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5 kama inavyoeleza sera ya afya ya mwaka 2007 "alisema.Shonza.
Alisema anaamini kwa sasa.baada ya kuondole wa baadhi ya watumishi katika hospitali hiyo hak una lugha mbaya kwa wagonjwa na kuwataka kwenye vikao vya kitumidhi wawe wanalikemea suala hilo kupunguza malalamiko.
Baada ya kutoa nasaa hizo Mbunge Shonza aliga wa mashuka 40 Vyandarua 40 , Madishi, Sab uni, Kanga pamoja na Pampasi kwa akina mama waja wazito vikiwa na thamani ya Milioni 3.1.
Alisema ameamua kutoa misaada hiyo kutokana na umuhimu wa akina mama pia akiunga juhudi za Rais Dkt, Samia Suluhu kwa kazi kubwa anay oifanya hasa katika.sekta.ya afya akiwapa Milioni 900 kujenga jengo jipya la mama na mtoto.
Sophia Simbeye mjamzito aliyekuwepo hospitalini hapo alisema sera ya nchi katika udara yanafya isemayo mama mjamzito na mtoto chini ya miaka 5 kutibiwa bure haifuatwi kwani wamekuwa wakia mbiwa wakanunue dawa madukani.
Alisema wananchi wengi wamekuwa na bima ya 30.000 lakini wakifika hospiyalini wanapewa daw a za bei ya chini ikiwemo panado,dawa za bei ya juu wanaambiwa wakanunue nadukani hali inayo sababisha wengi kutokata bima wakiiona haina faida.
Anne Mtafya mjamzito alisema amepata taarifa ujio wa fedha hizo anaomba ujenzi ukamilike hara ka ili wahepuke kubanana kwenye jengo hilo na wapatiwe vitanda wahepukane na kubanana.
Mganga mfawidhi wa hospitalii hiyo Dkt,Kelvin Masea alisema kitendo cha wajawazito na watoto chini ya miaka 5 kutozwa fedha kwa sasa halipo na wamekuwa wakitoa elimu na kugawa.nba ya simu kwa wanaokuja kutibiwa ili watoe taarifa..
Kuhusu uchakavu na ufinyu jengo la mama na mt oto alisema serikali imetoa Milioni 900 kujenga jengo jipya hivyo kukamilika kwa jengo hilo kutak uwa ni muarobaini tosha kwani vitanda vya kisasa vitawekwa.
Diwani wa kata ya Vwawa George Kiwaya (Must achi) alisema anampongeza mbunge Shonza.kwa msaada huo huku akisema wasinge katazwa kuse ma mitano tena angesema kutokana na kazi kub wa anayoifa nya akiunga juhudi za Rais Dkt, Samia.
Mbunge Shonza katika ziara yake kutembelea hospitali hiyo aliungana na mwenyekiti wana wak e ccm mkoa Emiliana Mwakyoma,menyekiti wan awake ccm Mbozi Jenny Chaula na katibu wake pamoja na viongozi wengine na wanachama.




Comments
Post a Comment