WATUMISHI MADINI WATEMBELEA MGODI WA BULYANHULU

 


#Katibu Mkuu Madini aanza Utekelezaji Maazimio
Timu ya Watumishi wapatao 13 kutoka kada mbalimbali
za Wizara ya Madini ikihusisha Makatibu Mahususi,
Watunza Kumbukumbu na Wahudumu wametembelea
Mgodi wa Barrick - Bulyanhulu uliopo Wilaya ya Kahama
Mkoani Shinyanga.
Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio na ahadi
alizotoa Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali
wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo
lililofanyika mwezi Mei, 2023, jijini Dodoma.
Aidha, ziara hiyo inalenga kuwajengea uelewa wa pamoja
watumishi wote wa Wizara kuhusu shughuli zinazofanywa
katika Sekta ya Madini hususan shughuli za uchimbaji wa
madini katika migodi mikubwa, ya kati na midogo ili
kuwezesha malengo mahususi ya wizara kutekelezwa kwa
pamoja kama familia moja ya Madini.
Watumishi hao wamepata fursa ya kutembelea maeneo
mbalimbali katika mgodi huo ikiwemo mgodi wa chini
( underground mining), sehemu ya uchenjuaji
(processing plant) bwawa la huifadhi tope sumu ( TSF) ,
sehemu ya upokeaji na utunzanji wa vifaa vinavyotumika
katika mgodi pamoja na kutembelea miradi ya jamii
inayotekelezwa na migodi hiyo kupitia Mpango wa
Uwajibikaji wa Migodi kwa Jamii (CSR).
Hili ni kundi la kwanza la watumishi wa kada hizo
kutembelea maeneo ya migodi ili kujionea shughuli
mbalimbali zinazofanywa. Kundi lingine la watumishi
kutoka kada hizo linatarajiwa kutembelea migodi
mbalimbali mapema mwezi Septemba.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa