‘Kuweni na subira ripoti takwimu hali ya ulemavu ‘


OFISI ya Taifa ya Takwimu imewataka wadau wanaohitaji ripoti za
takwimu za hali ya ulemavu nchini  baada ya matokeo ya sensa ya
watu na makazi ya mwaka 2022 kuwa na uvumilivu kwani bado
taarifa zake zinaandaliwa.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Takwimu Mkoa wa Tanga Toni
Mwanjota kwa niaba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali  Albina Chuwa,
wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya matokeo ya sensa ya watu na
makazi ya mwaka 2022 Kwa viongozi,watendaji na watu wa makundi
maalum mkoani Tanga.

Amesema kuwa matokeo ya ripoti hiyo yamekuwa yakisubiriwa kwa
hamu kubwa na wadau mbalimbali ,Ili kujua hali halisi ya kundi hilo
kwa sasa hapa nchini.

“Taarifa za watu wenye ulemavu ni ripoti ambayo inaandaliwa hivyo
tunaomba subira kutoka kwa wadau wote wa takwimu za hali za
watu wenye ulemavu,”amesema Mwanjota.

Amesema kuwa  ofisi ya takwimu inaelewa umuhimu wa ripoti hiyo
ndio maana imo katika orodha ya taarifa ambazo zinaandaliwa kama
ambavyo zilizotangulia hapo awali.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa