Wananchi Dar kupimwa magonjwa ya moyo



TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Hospitali ya Dar Group
wanatarajia kufanya kambi maalum ya upimaji na matibabu ya
magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na
mikoa ya jirani –
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na
Mawasiliano, Anna Nkinda imesema upimaji huo utafanyika kwa
watoto na watu wazima kuanzia Septemba 02, 2023 hadi Septemba
03,2023 kuanznia saa mbili asubuhi  hadi saa 10 alasiri jioni katika
Hospitali ya Dar group iliyopo Temeke .
“Aidha katika kambi hii kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao
watatoa elimu ya lishe bora, ambayo itawapa wananchi uelewa na
kufuata mtindo bora wa maisha na kuepukana na magonjwa
yasiyoambukizwa yakiwemo ya moyo, ambayo yanaweza kuepukika
kwa kufuata ushauri wa kitaalamu,”ameeleza Nkinda.

Amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao kujua
kama wana matatizo ya moyo, ili kuanza matibabu mapema kwa
atakayegundulika kuwa na magonjwa na kusisitiza kuwa huduma hiyo
itakuwa ya kuchangia gharama ya matibabu.

“Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0754578190  ya Dk
Tulizo Shemu,0684345921, Flaviana Masegesa na 0674179036 ya
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group,”
amesema.

Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa