TBS YAWAONYA WANAOFOJI NEMBO YAO
- Get link
- X
- Other Apps
Shirika la viwango Tanzania TBS limesema halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwapiga faini ya shilling million 20 wajasiliamali na wasindikaji watakao bainika kufoji nembo ya TBS pamoja na kuingiza sokoni bidhaa zisizokuwa na ubora.
Hayo yamebainishwa na kaimu meneja wa shirika la viwango Tanzania Tbs kanda ya Magharibi Rodney Alananga wakati akitoa elimu kwa wajasiliamali, wasindikaji na wamiliki wa viwanda na kufanyika katika ofisi za kata ya Matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa,Ambapo aliwataka waandaji wa bidhaa kuzingatia weledi na viwango na ubora wakati wa uandaaji wa bidhaa kabla ya kuingizwa sokoni.
‘’Tbs inazo skimu mbalimbali za udhibiti ubora ikiwemo skimu ya alama ya ubora,mzalishaji ambaye bidhaa yake imethibitishwa ubora kwa kuzingatia kiwango cha kitaifa cha bidhaa husika hupewa leseni ya kutumia alama ya TBS katika bidhaa hiyo hivyo kwa mwaka 2024 mzalishaji yeyote ambaye atashindwa kuwa na alama hiyo kwenye bidhaa yake atazuiliwa bidhaa yake kuingizwa kwenye maonesho makubwa ikiwemo nane nane na saba saba. Alisema. – Alananga.
- Get link
- X
- Other Apps


Comments
Post a Comment