WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MPIMBWE WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA BILIONI 1.2
Na Walter Mguluchuma,Katavi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Katavi imewafikisha Mahakamani watumishi saba wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi akiwemo mtunza hazina wa Halmashauri hiyo kwa kutuma za wizi wa zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 walizokuwa wakiziingiza kwenye akaunti za watu binafsi .
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Katavi imewafikisha Mahakamani watumishi saba wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpibwe Mkoani Katavi akiwemo mtunza hazina wa Halmashauri hiyo kwa kutuma za wizi wa zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 walizokuwa wakiziingiza kwenye akaunti za watu binafsi .
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine Maijo amewataja watuhumiwa hao waliofikishwa Kizimbani na Takukuru Mkoa wa Katavi kuwa ni Canuthe Matsindiko, Michael Katanga(Big),Masami Mashauri ambae ni mweka hazina wa Halmashauri hiyo(DT) Tumaini Misese,Maila Oluomba , Emanuel Salanga na Laurent Sunga.
Maijo alisema watuhumiwa hao wamefikishwa Mahakamani na kusomewa mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi na kusomewa mashitaka na mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Gwai Sumai
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi,Faustine Maijo akieleza mbele ya waandishi wa Habari juu ya kufikishwa Mahakamani kwa watuhumiwa saba wa Halmashauri ya Mpimbwe.
Amesema kuwa watuhumiwa hao saba kati yao watumishi wa Halmashauri ya Mpimbwe ni watano na mmoja na wamanispaa ya Mpanda na mwingine alikuwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa sasa yupo Shirika la masoko Kaliakoo.
Amebainisha kuwa kabla ya kukamatwa kwa watumishi hao Takukuru Mkoa wa Katavi walipokea taarifa juu ya ubadilifu wa fedha katika Halmashauri ya Mpimbwe ulikuwa ukihusu wizi wa fedha kiasi cha Tshs 1,232 869,000 fedha hizo zikuwa kwenye akaunti ya Halmashauri ya Mpimbwe na walizifuja kwa kusingizia kuwa waliwalipa wakandarasi ambao walifanya shughuli mbalimbali jambo ambalo halikuwa na ukweli .
Maijo alisema uchunguzi waliofanya wamebaini fedha hizo walizilipa kwa watu binafsi ambao hawakuwa na kazi yoyote walizofanya katika Halmashauri hiyo lakini waliwalipa watu ambao walikuwa wakifahamiana nao kwa kibali kuwa wamewalipa wakandarasi waliokuwa wakifanya kazi za ukandarasi mbalimbali .
Watumishi hao wamefikishwa Mahakamani na kusomewa mashita matatu shitaka la kwanza wameshitakiwa kujihusisha na genge la uhalifu shitaka la pili ni la uhujumu uchumi na shitaka la tatu ni wizi .
Mwendesha mashitaka wa Takukuru Mkoa wa Katavi Kelvin Mwaja alisema wamewafungulia mashita watuhumiwa hao wote saba kesi namba tano ya uhujumu uchumi ya 2023 katika Mahakama ya Hakimu ya Mkazi Katavi.
Washitakiwa hao kwa pamoja wameshitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi kinyume cha aya ya nne [c ]na kifungu cha 57(1) 60 ( 2 ) cha sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya 2022 washitakiwa hao wote wanadaiwa kama watumishi wa Halmashauri hiyo kwa pamoja waliunda genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia manufaa walifanya matukio kwa mtililiko kwa lengo la kufanana na kujipatia manufaa ya kiasi hicho cha fedha .
Shitaka la pili wanashitakiwa washitakiwa kwa kosa la kuisabishia Halmashauri hasara kinyume na kosa la kifungu cha sheria sura ya 10(1) na 57 [1] na 60[2] sura ya 200 Marejeo ya 2022
Kosa la taui ni wizi ambalo wameshitakiwa kinyume na kifungu cha sheria namba 265 na 270 kinyume na kifungu kanuni ya adhabu sura marejeo ya 2022 kwa pamoja wanadaiwa kuiba kiasi cha shilingi Bilioni 1.2 kwa kuwa ni watumishi wamekiuka kifungo cha sheria namba 270 kwa kufanya wizi wakiwa watumishi wa umma
Watuhumiwa hao baada ya kusomewa mashita waliambiwa na Mahakama kuwa hawatakiwi kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Katavi haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi mpaka mahakama ya juu zaidi ya hiyo .
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Katavi Gwai Sumai alihairisha kesi hiyo hadi hapo septemba 4 na watuhumiwa hao wote saba waliamriwa kwenda katika gereza la mahabusu la Mpanda mjini hadi hapo siku ya tarehe hiyo
Mwisho


Comments
Post a Comment