DKT. KIRUSWA AITAKA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MAKAA YA MAWE KUCHANGIA HUDUMA KWA JAMII RUKWA


Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa
ameitaka Kampuni ya uchimbaji wa Kati wa Makaa
ya Mawe ya Edenville Tanzania Limited kuchangia
huduma kwa jamii inayozunguka eneo la shughuli
za uchimbaji wa madini hayo kama Kanuni chini ya
Kifungu namba 129 cha Sheria ya Madini
kinavyoelekeza.

Hayo, ameyasema wakati akizungumza na
wananchi wa Kata ya Pande Kijiji cha Komolo
wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa kwenye mkutano
wa hadhara ambapo amesisitiza kampuni hiyo
kuwasilisha Mpango wa Wajibu wa Mmiliki wa
Leseni ya Madini kwa Jamii inayozunguka Mgodi.

"Naomba mkutane na Halmashauri ya Wilaya ya
Nkasi ili kupata vipaumbele vya eneo husika ili
mjue mnatakiwa kuchangia katika maeneo gani,
uchangiaji huo sio ombi bali ni takwa la kisheria
kwa mmiliki wa leseni kuchangia huduma za
kijamii inayozunguka mgodi", amesema Dkt.
Kiruswa.

Aidha, Dkt. Kiruswa ameliagiza Shirika la Madini la
Taifa (STAMICO) kuitembelea Kampuni ya Edenville
Tanzania Limited ili kuona namna bora ya
kushirikiana nayo kwa lengo la kusaidia na
kuongeza tija kwenye uzalishaji wa madini hayo.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kiruswa ameitaka
Kampuni ya Edenville Tanzania Limited inayomilki
hisa kwa asilimia 90 kuachana na migogoro na
mbia mwenza mwenye hisa ya asilimia 10 ambapo
amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano na kila
mmoja kupatiwa haki yake kwa mujibu wa
mkataba waliyowekeana.

Awali, Dkt. Kiruswa alitembelea Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa kwa lengo la kupata taarifa za
shughuli za Sekta ya Madini zinazoendelea
kufanyika Mkoani humo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Makongoro Nyerere amempongeza Dkt. Kiruswa
kwa kufanya ziara katika mkoa huo na kumuomba
kuwapa moyo wachimbaji wa madini ili kuchochea
maendeleo ya sekta hiyo.
Baadhi ya viongozi walioshiriki ziara hiyo ni
pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter
Lijuakali, Mwakilishi wa Kamishna wa Madini
Mhandisi Shija Itandiko, Kaimu Afisa Madini Mkoa
wa Rukwa Masia Gabril, Mwenyekiti wa
Wachimbaji Wadogo wa Madini wa Mkoa wa
Rukwa Masie Mambegele na Meneja Kampuni ya
Edenville Tanzania Limited inayomilki mgodi wa
Makaa ya Mawe Darwesh Gamdust.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa