Mbaroni kwa kuua mke, shemeji
TANGA; JESHİ la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kumkamata
Swalehe Miraji Ally, mwenye umri wa miaka 38 aliyekuwa kakimbilia
mkoani Tabora baada ya kufanya mauaji ya mkewe na shemeji yake
kwa kuwakata na mapanga mara mbili kichwani wakati wakiwa
shambani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema
kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni fundi ujenzi mkazi wa Mkanyageni
wilayani Muheza, alimuua mkewe Mwanahawa Hassan (24) na Sauda
Sufian (20) kisha kukimbilia Tabora, ambapo jitihada za Polisi
zilifanikiwa kumkamata.
Katika tukio linguine polisi imemkamata mkazi wa Handeni, Rajab
Athuman mwenye umri wa miaka 32 akituhumiwa kumuua kwa
kumkata kichwa kwa kutumia kamba ya katani Helena Sila.

Comments
Post a Comment