RAIS DKT,SAMIA NI MTU NA NUSU RAIS WA WAKANDARASI WANAWAKE WAZAWA NCHINI



Na Ibrahimu Yassin,Songwe

RAIS wa wakandarasi Wanawake wazawa nchini Judith Odunga leo amesemea Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu ni mtu na nusu kutokana na kuwaheshimisha wakandarasi wanawake kwa kuwapa tenda za kujenga miradi ya barabara ambayo awali ilifanywa na wanaume pekee.

Odunga amesema wanawanachama 460 nchi nzima ambao wanajihusisha na ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara,madaraja na makaravati ambapo awali baada ya kujisajili walipeleka hoja ya utambuzi kwa Rais Samia wakati akiwa Makamu.

Amesema baada ya Rais Dkt,Samia kuwa Rais kamili,alikubali hoja zetu na kuwapatia ujenzi wa barabara kilometa 20 zilizopo mkoani Songwe kama kipimo huku akijinasibu kuishangaza Dunia kwa kujenga barabara yenye viwango vya juu.

Amesema ujenzi wa barabara ya Lami kilometa 20 waliyopewa mkataba wake ni wa mwaka mmoja ambapo wao wamejipanga kuikamilisha kabla ya wakati na kwa ubora wakiwa na lengo la kupewa kilometa nyingi Zaidi.

‘’Kulikuwa na hoja kuwa wanawake hatuweza ,lakini sasa tunataka kuionesha Dunia kuwa tunaweza,tunajenga mradi huu usiku na mchana ili tumalize kabla ya muda tuliopangiwa ili kujenga Imani na kupewa miradi mingine mikubwa zaidi’’amesema Odunga.


Amesema wakati wanafika eneo hilo walipata mapokezo mazuri na ushirikiano kwa wananchi,na wao kuwapa ajira za upishi,uchotaji wa maji na vibarua vingine huku vifaa vingine vya ujenzi wakinunua katika maduka yanayozunguka vijiji hivyo na kuufanya mradi kuwa faraja kwao.

‘’Wananchi wameuona mradi huu kuwa faraja kwao,vifaa vyote yakiwemo Mafuta ya kuweka kwenye magari tunanunua hapahapa n ahata mahitaji yote tunanunua kwenye maduka ya wenyeji na kuufanya mzunguko wa fedha kuwa mkubwa’’amesema Odunga.


Nae Mhandisi Hilda Mwatelemo amesema anakila sababu ya kuipongeza serikali kwa kuwapa kazi hiyo huku akipongeza usimamizi wa karibu wa wizara ya ujenzi na timu ya Tanroads HQ kwa ushirikiano mzuri huku akisema kila kilometa 5 wameungana kampuni 3 watahakikisha wanakamilisha ujenzi kwa wakati.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa