Maafisa maendeleo ya jamii Nkasi wakabidhiwa Pikipiki
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Halmashauri ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imekabidhi pikipiki mbili kwa Maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata kwa lengo la kurahisisha majukumu yao ya kuwahudumia Wananchi.
Akikabidhi Pikipiki hizo kwa Maafisa maendeleo ya jamii wa kata za Kizumbi na Ninde kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Nkasi Valeriana Mwampasi amewataka Maafisa hao kuzitunza vyema Pikipiki hizo na kuzielekeza kwenye matumizi sahihi Ili ziweze kutoa huduma kwa Wananchi wanaoishi katika kata hizo.
Amesema kuwa lengo la wizara ya maendeleo ya jamii na makundi Maalum kutoa Pikipiki hizo ni kutaka jamii ifikiwe kwa haraka na uhakika hivyo Ni muhimu kwa Pikipiki hizo kutunzwa vyema Ili ziweze kutoa huduma kwa jamii kwa muda mrefu.
Awali Afisa maendeleo ya jamii wilaya ya Nkasi jumaa AweSo amezitaja kata hizo Kama zilizo katika mazingira magumu na ndiyo maana walionelea wapewe Pikipiki hizo Ili ziwarahisishie kazi zao kwa kuweza kuwafikia Wananchi wengi zaidi.
Hivyo Sasa amewataka matokeo chanya kufuatia kukabidhiwa Pikipiki hizo kwani sasa imani yao kwao Ni kubwa katika kuhakikisha jamii inahudumiwa.
Kwa upande wao Maafisa maendeleo ya jamii wa kata hizo za Kizumbi na Nide Credo Salvatory Khamis na Henry Lawrent Khamis wameipongeza serikali kwa hatua zilizochukuliwa kwa kuwapatia Pikipiki hizo hasa kutokana na kata hizo kuwa katika mazingira magumu kutokana na Jiografia waliyopo



Comments
Post a Comment