WAKULIMA ILEJE –MBOZI WAMPA 5 RAIS DKT,SAMIA UJENZI BARABARA YA LAMI RUANDA IDIWILI HADI ITUMBA.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
‘’Tulilazimika kuuza mazao kwa walanguzi kutokana na barabara kuwa mbovu,ujenzi huu ukikamilika tutaongeza usalishaji na kuuza bei ya juu kwenye masoko ya nje ya mkoa’’
WAKULIMA katika wilaya za Ileje na Mbozi wameipngeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga baraara ya Lami katika maeneo yao ambayo ni bingwa kwa kilimo cha mazao mbalimbali na ufugaji ikiwemo upasuaji na usafirishaji wa mbao.
Serikali inatekeleza Ujenzi wa barabara ya Ruanda-Nyimbili-Hasamba-Izyila hadi Itumba wa kilometa 76.67 na Mahenje – Hasamba hadi Vwawa-kilometa 31.9 ni barabara iliyounganisha Vwawa na Tunduma ikiwa ni muhimu katika shughuri ya kiuchumi na kijamii.
Ujenzi huo ukikamilika utachochea na kuongeza thamani ya kiuchumi hasa kwa wakulima ambao wengi wao wanalazimika kuuza mazao yao kwa bei ya chini kutokana na kushindwa kumudu ghamarama za usafirishaji wa mazao kwenda kwenye masoko yaliyopo nje ya mkoa.
Wakizungumza leo kwa nyakati tofauti,wakulima hao,wamesema kwa sasa wameanza kuongeza uzalishaji kwa kulima mashamba mengi wakiwa na uhakika wa kupata mavuno mengi watakayosafirisha kwenda mikoa mbalimbali kuuza kwa bei ya juu kutokana na ujenzi wa barabara hizo.
James Mwashilindi mkazi wa Itumba amesema wilaya ya Ileje inasifika kwa kilimo cha miti ambapo wamekuwa wakipata shida kusafirisha hasa nyakati za mvua kutokana na ubovu wa barabara huku wakitozwa fedha nyingi pindi wanapo kodi gari.
Amesema kukamilika kwa barabara hizo kutapelekea bei ya kukodi magari kupungua kutokana na wataweza kuzifikisha kwa wakati katika eneo la soko na kwamba wakata wa barabara Tanroads chini ya wizara ya ujenzi inafanya kazi kubwa kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.
Suma Kayange mkazi wa Mahenje amesema wilaya ya Ileje na Mbozi ni wakulima wakubwa wa mazao ya chakula na pia wanapkea mazao na bidhaa nyingine toka nchi jirani ya Malawi,hivyo kukamilika kwa barabara hizo kutarahisisha usafirishaji wa mazao yao na kuongeza tija za kiuchumi.
Awali akizungumza na waandishi wa habari,ofisini kwake, meneja wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoani Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga alisema ujenzi wa barabara hizo umefadhiriwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania chini ya wizara ya ujenzi kupitia wakala wa barabara Tanzania.
Amesema watahakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyowekwa ili thamani ya fedha iendane na ualisia wa mradi na kuwa hawatalala na watahakikisha hakuna kasoro itakayojitokeza kwenye ujenzi huo.
Mbali na ujenzi wa mradi huo,pia kuna mradi mungine wa ujenzi wa barabara ya Ruanda- Idiwili kiwango cha lami kilometa 20 unaojengwa na wakandarasi wazawa wanawake kwa Shilingi Bilioni 45 ambao umefikia asilimia zaidi ya 20 ujenzi ambao unasubiriwa kwa hamu na wakazi wa eneo hilo.



Comments
Post a Comment