WANANCHI WAWAHARAKISHA WAKANDARASI WANAWAKE WAZAWA KUKAMILISHA MRADI KWA WAKATI.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
WANANCHI katika vijiji vilivyopo wilaya ya Mbozi na Ileje mkoani Songwe,wamewaharakisha Wakanda rasi wanawake wazawa kukamilisha ujenzi wa barabara kwa wakati wakiwa na uchu wa kukuza uchumi kwenye sekta ya usafirishaji mazao.
Wamesema wamejipanga kuhakikisha wanaitumia barabara hiyo kukuza uchumi kwa kusafirisha bidhaa kutoka mashambani kwenda kwenye masoko yaliyopo nje ya mkoa wa Songwe wakitumia barabara hiyo hali iliyopelekea wawe na uchu wakitaka ujenzi ukamilike.
Serikali ya Tanzania ilitoa kiasi cha shilingi Bilioni 45 kujenga barabara ya Lami kilometa 20 kuanzia Ruanda hadi Idiwili ikiwa na lengo la kuondoa changamoto ya mindombinu ya barabara na kukuza uchumi kwa jamii.
Katika ujenzi huo makampuni manne ya wanawake wazawa walipewa tenday a ujenzi ambapo kila kampuni ilipewa kilometa 5 huku yakiungana kuongeza nguvu ya pamoja kujenga mradi huo ambapo wamejinasibu kukamilisha kabla ya muda uliowekwa.
Sehemu ya kwanza ya ujenzi ni Ruanda -Idiwili ikijengwa na M/s ULM—HIGO-TANZHON INVESTMENT JV LIMITED, na sehemu ya pili inajengwa na M/s AB,Msengi-Hystem na Msetti Women Contractor Joint Venture.
Sehemu ya 3 ya ujenzi inajengwa na M/s Ibra Contractors.Nail it Constructution limited and Kimango Engineering Company na sehemu ya nne ya ujenzi inajengwa na M/s Judex Contractors, Cyfloa 2020 Compan limited, ML Smart Compan Limited.
Ujenzi wa barabara hiyo ya Lami Ruanda Idiwili kwa kiwango cha Lami kilometa 20 ni moja ya mikakati ya serikali kuharakisha maendeleo ya kichumi na kijamii mkoani Songwe na maeneo jirani kwa kuboresha mtandao wa barabara ili kuongeza ufanisi sekta ya usafirishaji.
Safina Mtafya Mkazi wa njia panda Iyula amesema tayari wawekezaji ikiwmo wajasiliamali wameanza kufika kwenye vijiji hivyo kufungua biashara na kwamba endapo ujenzi utakamilika kwa wakati wanauhakika uchumi utakuwa kwa kasi.
Sanke Simfukwe mkazi wa Idiwili amesema katika vijiji hivyo wakulima wengi wataongeza thamani ya mazao yao kutokana na barabara hiyo kwani hata bidhaa kutoka nchi jirani ya Malawi zikiwemo Mbao kutoka Ileje zitapita katika barabara hiyo kwenda mikoani.
Rais wa wakandarasi wazawa nchini Judith Odunga amesema serikali ya Rais Dkt,Samia imewaamini na wao hawataiangusha watahakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa wakati na kwa viwango vya juu huku lengo lao ni kutaka kujenga miradi yenye thamani kubwa zaidi.




Comments
Post a Comment