Maafisa ugani Nkasi watakiwa kutoa elimu ya kilimo kwa Wakulima wakati huu wa masika


Na Asha Hassan,Nkasi

Afisa kilimo, Mifugo na Uvuvi (W) Nkasi, Mkoani Rukwa Dkt.John S. Tlatlaa amewataka Maafisa Ugani wilayani humo kuendelea Kutoa elimu ya kilimo cha Ufuta na Mbaazi kwa wakaazi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika na kata zingine zilizofanyiwa utafiti kwa ajili ya kilimo cha mazao hayo.

Akizungumza katika kikao kazi cha maandalizi ya msimu wa kilimo kwa mwaka 2025/2026, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya (W) Nkasi Novemba 20, 2025, Dkt. Tlatlaa amesema kuwa Halmashauri imekusudia kuendeleza zao la Ufuta na Mbaazi kutokana na fursa za masoko ya mtandao uliopo.

"Kama tulivyoahidi kwamba kutakuwa na mashamba darasa kadhaa kama 39 kwa maeneo yote ya kata za mwambao amabayo yataanzishwa kwa mwaka huu katika mazao ya Ufuta kwa hiyo wale Maafisa kilimo wa hizo kata katika maeneo yenu mnapokutana kwenye vikao hata vile vya Kijiji basi muendelee Kutoa elimu ya watu kulima zao la Ufuta lakini pia waandae mashamba ya Ufuta "
Aidha amewaomba Maafisa kilimo hao kumsaidia Mkurugenzi kukusanya mapato kupitia wafanya biashara wanaokwenda na Malori kwenye maeneo yao kuhakikisha wanalipa tozo zinazotakiwa kwa kulipa ushuru huku akiwaeleza kuwa wasisite kuyakagua Malori hayo pamoja na kutoa taarifa kwa watendaji endapo watabaini kama Malori hayo hayajalipa ushuru ili Halmashauri ifikie malengo yake ya kufikisha huduma kwenye jamii.

Sambamba na hayo amewataka Maafisa hao wa kilimo kwenda kuyafanyia kazi yale yote waliyoyajadili kupitia kikao kazi hicho ili kufikia malengo yaliyokusudiwa

Mkuu wa sehemu ya kilimo Emmanuel Gamasa amesisitiza kuwa Maafisa kilimo wote waongeze kasi ya usajili wa wakulima kwenye mfumo wa pembejeo za ruzuku pamoja na kuwashauri wakulima kwenye maeneo yao kutumia kanuni bora za kilimo.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa