WANAKIJIJI 240 WAPATA AJIRA KATIKA UJENZI WA BARABARA YA LAMI RUANDA IDIWILI,WASIFU USIMAMIZI WA TANROADS.
Na Ibrahim Yassin,Songwe
WANAKIJIJI Zaidi ya 240 wanaozunguka mradi wa ujenzi wa barabara ya Ruanda Idiwili wilayani Mbozi mkoani Songwe wamepata ajira za mikataba za kufanya kazi mbalimbali huku wakipata fedha zinazoendasha Maisha yao ya kila siku.
Wakizungumza leo kwa nyakati tofauti katika vijiji hivyo,wamesema ujio wa mradi huo umekuwa ni fursa kwao kwani wamepata ajira na kujipatia kipato huku vijiji hivyo vikiendelea kupanda thamani hasa katika sekta ya ardhi kutokana na watu wengi kununua maeneo ya uwekezaji.
Rashford Mtafya mkazi wa Iyura amesema awali viwanja vya kujenga nyumba za makazi vilikuwa vikiuzwa kati ya laki 4 hadi 5 laikini kwa sasa vinauzwa Zaidi ya milioni 2 kutokana na ujio wa barabara hiyo.
Jangson Mwamengo mkazi wa Idiwili amesema pindi barabara hiyo itakapo kamilika vyombo vya moto vitaongezeka na nauli zitapungua kwani kwa sasa wanalazimika kutoa nauli isiyorafiki kutokana na changamoto ya barabara.
Amesema sambamba na hilo,pia wamefurahi kuona vijana wao wamepewa ajira za mikataba kufanya kazi katika mradi huo huku akina mama lishe wakiongeza tija ya kupika vyakula kuwauzia wafanyakazi wa wanaojenga mradi huo na kuongeza uchumi.
Debora Sengati katibu wa chama cha wakandarasi wanawake wazawa nchini, baada ya kupeleka maombi kwa Rais Dkt,Samia akiwa makam na alipopata urais akawaamini na kuwapa miradi na sasa watahakikisha hawatamuangusha watajenga kwa wakati kwa viwango bora.
Amesema walipoanza ujenzi wa mradi huo,wakisimamiwa kwa karibu na wakala wa barabara (Tanroads) mkoani Songwe wameweza kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 240 wanaozunguka mradi ambao kwa sasa wanafanya kazi zinazowapatia fedha huku wakifurahia mapokeo mazuri kutoka kwa wananchi na wazee wa mila.
Nae Mhandisi Hilda Mwatelemo,amesema wameungana kampuni zaidi ya moja lengo ni kujenga mradi kwa viwango huku wakiwa kama ni kipimo na wao watahakikisha wanafanya vizuri kuliko kampuni za wanaume wakiwana lengo la kupewa miradi mikubwa zaidi.





Comments
Post a Comment