Polisi Rukwa kuwasaka waliofukua kaburi na kuondoka na mwili wa marehemu



Na Israel Mwaisaka,Rukwa

Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linawatafuta Watu waliohusika kufukua kaburi la Julius Ladislaus (24) aliyefariki Novemba mwaka Jana na kuondoka na mwili wa marehemu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa Shadrack Masija alisema kuwa marehemu alifariki Novemba mwaka Jana wilayani Chunya mkoani Mbeya na mwili wake kusafirishwa mkoani Rukwa na kuzikwa Katika Kijiji cha Lunyala wilayani Nkasi.

Amedai kuwa mnamo February 14 ya mwaka huu wa 2025 mwili wa marehemu ulikutwa umefukuliwa Katika kaburi Hilo na mwili kuchukuliwa na kuliacha sanduku na kaburi lake vikiwa wazi huku mwili wa marehemu wakiondoka nao.

Hivyo amewaomba Wananchi wote walio na taarifa juu ya Watu waliofanya vitendo hivyo viovu na vya kutisha kutoa taarifa Polisi Ili Watuhumiwa waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kamanda Masija Alidai kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina juu ya suala Hilo na kuwa kimsingi suala Hilo linahusishwa na Imani za kishirikina na kuwasihi Wananchi kuacha a na Imani hizo ambazo katika kipindi hiki zimepitwa na wakati.

Sambamba na Hilo pia jeshi Hilo linamtafuta mtu ambaye Hadi sasa hajajulikana kuhusisha na kifo cha Mwanamke mmoja aliyekutwa amekua katika nyumba ya kulala wageni mjini Namanyere.

Alidai kuwa mnamo February 19,2025 Binti huyo mwenye umri wa miaka 19 akiwa na Mwanaume ambaye Bado hajajulikana alikutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni na kuwa baada ya kifo cha mwanamke huyo kijana huyo wa kiume alikimbia na Hadi sasa haijulikani alipo.

Hivyo ametoa wito kwa jamii kwa yeyote juu ya aliyetekeleza tukio Hilo watoe taarifa haraka kwenye mamlaka za serikali kwa ajili ya hatua mbalimbali za kisheria.

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa