Jamii yaombwa kutowahusisha Wazee na imani za kishirikina




Na Ibrahim Yassin,Songwe

Wananchi wa Kitongoji cha Hawiga Kijiji cha Shaji Kata ya Mlangali wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kuwahusisha wazee wa Kitongoji hicho na imani za kishirikina kwa kuwa vitendo hivyo hupelekea kutendewa.

vitendo vya ukatili mkoani Songwe vimekuwa vikishikAa kasi huku wazee wakishutum8wa kitu ambacho kinapingwa vikali na jamii huku jeshi la polisi likiendelee kuiasa jamii kuwapenda wazee.



Kauli hiyo ilitolewa Februari 25, 2025 na Polisi Kata ya Mlangali Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Robart Kasunga wakati akitoa elimu kwa wana nchi hao juu ya umuhimu wa kuwatunza na kuwalea wazee kwani kundi hilo kwa sasa ni hazina kubwa katika malezi bora ya jamii ya sasa.

"Acheni kuwahusisha wazee au watu wa makamu moja kwa moja na imani za kishirikina kufanya hivyo ni kosa kisheria na atakayebainika kufanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo" alisema Mkaguzi Kasunga.



Sambamba na hilo, Mkaguzi Kasunga amewataka wananchi wa Kitongoji hicho, kutoa misaada mbalimbali kwa wazee hao ikiwa ni pamoja na mahitaji yao muhimu ili wajione wapo karibu na jamii na kuyafurahia maisha yao ya kila siku Kijijini hapo.

Ikumbukwe kuwa baadhi ya watu wanapowaona wazee wenye umri mkubwa wanadhani kuwa ni washirikina kitu ambacho hakina ukweli wowote.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa