Halmashauri ya wilaya Nkasi yaweka mkakati wa kukabiliana na uhaba madawati
- Get link
- X
- Other Apps
KAIMU mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa Steward Vidoga amesema kuwa halmashauri katika kukabiliana na changamoto ya madawati shuleni wametenga Tshs,Mil.80 kutokana na mapato ya ndani na mchakato wa utengenezaji wa madawati huo wa madawati unaendelea.Ameyasema hayo jana alipokuwa akijibu swali la papo kwa hapo kutoka kwa diwani wa kata ya Chala Michael Mwanalinze aliyetaka kujua halmashauri Ina mpango Gani wa kupunguza tatizo la madawati Katika shule za msingi na sekondari ambapo amedai kuwa Hadi sasa katika utengezaji wa viti na meza na katika awamu hii ya kwanza ambayo itakamilika mapema wiki ijayo kwa kukamilisha utengenezaji wa viti na meza 506.Amesema kuwa wiki ijayo wakikamilisha awamu hiyo ya kwanza wataanza kuyatengeneza madawati mengine Ili kuweza kukamilisha Tshs,mil.80 iliyotengwa Katika mwaka huu wa fedha wa 2024-25.Vidoga amefafanua kuwa halmashauri inatambua changamoto kubwa ya madawati katika shule zote za msingi na sekondari na kuwa halmashauri itaendelea kutenga fedha zaidi katika bajeti yake ya 2025-26.Pia katika baraza Hilo la Madiwani iliibuka hoja ya matibabu Bure kwa Wazee,Watoto na Wajawazito lilioulizwa na diwani wa kata ya Kipundu Kudra Ahmed ambapo kaimu mganga mkuu wa wilaya Jesepha Joseph alidai kuwa matibabu ya Bure kwa kada hizo za watu yapo ingawa ameshauri kuwa mwarobaini wa changamoto hizo za matibabu ya Bure ni Watu kuwa na bima ya afya.Amefafanua kuwa mtu akiwa na bima ya afya itamuhakikishia Kila mwananchi kuwa na uhakika wa matibabu,hivyo ni vyema jamii ikajielekeza kwenye mpango wa bima Kila mmoja badala ya kusubiri kutibiwa kwa fedha taslimu na mwishowe Watu kusubiri kutibiwa Bure kwa huruma za visingizio vingi.Pia baraza Hilo la Madiwani limeweza kupitisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2025-2026 ya Bil.38.9 ambapo katika makadirio hayo ruzuku kutoka serikali kuu ni Bil.35.6,Makusanyo ya ndani Bil.3.3 na hivyo kupata jumla ya Bil.38.9
- Get link
- X
- Other Apps



Haifunguki kbs
ReplyDelete