UTATU MTAKATIFU WA VIONGOZI CHANZO SONGWE KUPAA KIMAENDELEO.




"Tumekuwa tukifuata ushauri kwa Dc,uongozi wa mkoa na uongozi wa Chama,tunakusanya vizuri mapato na miradi inasimamiwa vizuri"

Na Ibrahim Yassin,Songwe 

WANANCHI wa vijiji mbalimbal wilayani Songwe mkoani hapa wameupongeza uongozi wa halma shauri hiyo kwa ukusanyaji mapato na nidhamu nzuri ya matumizi.

Nidhamu nzuri ya matumizi ya fedha imepelekea miradi ikamilike kwa wakati na kuifanya Songwe ipae kimaendeleo 

Johnson Samson mkazi wa Mkwajuni amesema amekuwa akifuatilia kwa mbali jinsi halmashauri inavyoendeshwa amekundua hali ya maendeleo ilivyo.



Amesema kila mradi unaojengwa umekamilika kwa wakati na hakuna malalamiko baina ya waka ndalasi na viongozi wa halmashauri ukilinganisha na halmashauri zingine.

Amesema halmashauri zingine ndani ya mkoa wa Songwe ameshuhudia wakurugenzi wakidaiwa fedha na wakandalasi wazawa walizozitumia kukamilisha miradi kwa kuweka miundombinu husika.

Jamila Mwashilindi mkazi wa Iseche amessema  wilaya yanSongwe ni moja ya wilaya mpya mkoan i Songwe inayoenda kwa kasi kimaendeleo huku ushirikiano wa.viongozi ukiwa.mzuri.

Amesema mkurugenzi Kavishe, mwenyekiti Sam bila na mbunge Mulugo wametengeneza utatu mtakatifu huku wakipata ushauri wa mkuu wa wilaya Itunda na na uongozi wa Ccm na kuifanya wilaya kupaa kimaendeleo.

" makusanyo  mazuri ya mapato ya ndani, nidha mu ya matumizi kwenye miradi, ushirikiano uliopo kwa viongozi wa juu na watendaji chanzo halmas hauri hiyo kung"ara kimaendeleo "amesema. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe Secillia Kavishe amesema ni kauli za wananchi zinamashiko kwani Songwe ipo vizuri kimapato na.makusanyo.


Amesema malengo yao ni kuhakikisha wanakus anya vizuri na kuvuka lengo na kuwa takwimu za miaka mitatu zimeweka bayana namna walivyokusanya.

Kavishe amesema mwaka 2021/23 walikadilia  kukusanya Bilioni 2.93 lakini makusanyo halisi walikusanya Bilioni 2.94 sawa na asilimia 100, na mwaka 2022/23 walikadilia kukusanya Bilioni 3.4 lakini walifanikiwa kukusanya Bikioni 3.9 sawa na asilimia 113.

Ameongeza kuwa mwaka 2023/24 walikisia kukusanya  Tsh, Bilioni 4.2 lakini walikusanya Tshs, Bilioni 4.3 sawa na asilimia 102 huku mikakati ya kuvuka lengo la makusanyo kwa mwaka 2025 linatarajia kuwa kubwa.

Amesema mbali na makusanyo hayo pia wamekuwa na nidhamu nzuri ya matumizi na wakifuatilia vyema miradi na kuhakikisha inakamilika bila dosari.

"Ndugu mwanahabari, Songwe kwa sasa haika matiki kimaendeleo huku wakiufanyia kazi ushau ri wa viongozi wa wilaya na mkoa hali iliyofanya wilaya itulie na wananchi wakiendelea kupiga kazi" amesema. 

Mkuu wa wilaya ya Songwe Solomon Itunda anasema wamekuwa wakali pale wanapoona mambo yanakwama na amekuwa akitoa ushauri ili Songwe ipae kiuchumi.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa