RC MBEYA AMFANYIA TUKIO MMILIKI SHULE YA HOLLY LAND PRE AND PRIMARY SCHOOL CHUNYA.
Na Ibrahim Yassi, Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amefanya ziara ya kushtukiza akiitembelea shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Holly Land iliyopo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Makongolosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Mkuu huyo wa mkoa ameitembelea shule hiyo jana baada ya kufanya vyema kwa kufaulisha wanafunzi wote wa darasa la saba na kushika nafasi za juu hadi ngazi ya Taifa.
Lengo la kutembelea shule hiyo ni kuipongeza kwa matokeo mazuri tangu kuanzishwa kwake na uwekezaji mkubwa wa Lawena Nsonda(Baba Mzazi), huku akishauri jitihada zaidi zifanyike.
Shule hiyo imedaiwa kuuheshimisha mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla kutokana na kufau lisha wanafunzi wote kwa alama One na Two katika mitihani yote.
Aidha amewataka wazazi Mkoani Mbeya kuwa peleka watoto shuleni hapo badala ya kuwapeleka mikoa ya mbali kwani shule ina huduma nzuri na malezi mazuri wakiwemo walimu wabobezi.
^Mkurugenzi Lawena Nsonda unayejulikana kwa jina la umaarufu Baba Mzazi, shule yako imetuhe shimisha hivyo ongeza jitihada zaidi ili iongoze kitaifa katika mitihani ijayo^, alisema Rc Homela.
Kwa upande wake Lawena Nsonda (Baba Mzazi) ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoong ozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuto a fursa kwa wawekezaji nchini wakiwemo wamili ki wa Shule.
Alisema kwa kuwa serikali inatambua umuhim u.wa wawekezaji na wao wapo tayari kubuni mbi nu mpya kuongeza ufauru kuuheshimisha mkoa na Taifa kwa ujumla.
Shule ya Holly Land ni moja ya shule bora zinazof anya vema Kiwilaya ,Kimkoa na Kitaifa.ambapo mwaka huu wanafunzi karibu wote wamefauru kwa alama A na B.
.




Comments
Post a Comment