MSAADA WA KISHERIA WA MAMA SAMIA KUZINDULIWA RUKWA


Katibu tawala wa mkoa Rukwa Msalika Makungu

Na Israel Mwaisaka,Rukwa

SERIKALI mkoani Rukwa imetangaza kuzinduliwa kwa kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria  ya MAMA Samia Leagel Aid itakayozinduliwa siku ya kesho Feb. 25 majira ya saa 2 asubuhi katika viwanja vya stendi ya mabasi ya Sokomatola ambapo wananchi watapata msaada wa kisheria kutokana na changamoto mbalimbali zinazo wakabiri.

Akizungumzia uzinduzi wa Kampeni hiyo, Katibu tawala mkoa wa Rukwa Msalika Makungu amesema kuwa lengo la kampeni ni kutoa msaada kwa waathirika wa vitendo mbalimbali ambao wengi wao hawana uwezo wa kufikia huduma za kisheria hivyo wanapaswa kujitokeza kwa wingi ili wakapate huduma hiyo.

Aidha amesema kuwa huduma za kisheria zitakazo tolewa kipindi chote cha Kampeni zitakuwa ni bure ambapo kampeni hiyo itafanyika kwa muda wa siku tisa katika halmashauri zote za mkoa na baadhi ya kata katika mkoa wa Rukwa.

Kwaupande wake Beatrice Mpembo ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa haki za binadamu kutoka wizara ya Katiba na sheria amesema kuwa kampeni hiyo itakuwa ni endelevu licha ya kwamba itafanyika ndani ya siku tisa na kuongeza kuwa mama Samia Suluhu Hassan ameamua kuzitafutia ufumbuzi changamoto za wananchi ambao wamekuwa hawana uwezo wa kupata huduma za kisheria kwa kuanzisha kampeni hiyo.

Amesema kuwa mkoa Rukwa utakua ni wa 22 kufikiwa na huduma hii ya msaada wa kisheria kwani Hadi sasa mikoa 21 imefikiwa huku alidai kuwa wao wameona jinsi uhitaji wa kisheria unavyotakiwa katika maeneo mbalimbali Nchini huku akiwataka Wananchi kuzitumia vyema siku hizo 9 katika kutatuliwa changamoto mbalimbali walizonazo za kisheria.

Na amefafanua kuwa Leo wao wamekua na kikao kazi na Watendaji wa mpango huo kutoka katika wilaya zote tatu za mkoa Rukwa na kesho February 25 zoezi Hilo litazinduliwa rasmi na kuanza kazi ya utetezi Katika mkoa Rukwa

Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa