DC Itunda ampongeza DED Kavishe kwa ukusanyaji mapato na nidhamu ya matumizi


" Ushauti wangu katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya umezaa matunda Songwe sasa haikamatiki kimaendeleo"

Na Ibrahim Yassin, Songwe

Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Solomon Itunda jana alimpongeza mkurugenzi mtengmdaji wa halmashauri ya wilaya ya Songwe Secillia Kavishe kwa makusanyo mazuri ya mapato ya ndani na nidha mu ya matumizi.

Alisema anajisikia fahari kuwa na mkurugenzi msikivu ambaye anashaurika na kwamba amekuwa akisimamia vyema miradi na kuhakikisha fedha haipotei.

""Ded Kavishe ni mtu na nusu hivyo naona fahali kufanya kazi nae, miradi yote inatekelezwa vizuri fedha za umma hazipotei, anafanya kazi hadi muda wa ziada", alisema Dc Itunda.

Katika siku za hivi karibuni Itunda aliongoza Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Songwe (DCC ) Kujadili mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2025.

Mkuu huyo wa wilaya aliongoza Kikao kilichofanyi ka siku za hivi karibuni katika ukumbi wa Sambila uliopo katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Songwe.

Itunda katika kikao hicho aliwasisitiza watendaji wa Halmashauri kusimamia ukusanyaji wa mapa to na kuzingatia kanuni na sheria za matumizi ya fedha za umma.

Alisema kuwa msingi wa uendeshaji wa Halma shauri unategemea ukusanyaji wa mapato hivyo, ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kupitia vyanzo vilivyotengwa anakusanya mapato na kubuni mbinu mpya zitakazosaidia uingizaji wa mapato ya Halmashauri.

Pia, Kiongozi huyo wa Wilaya amesisitiza suala la uimarishaji mahusiano na upendo kati ya watend aji wa Serikali na wadau mbalimbali ili kuepuka migogoro mbalimbali inayotokana na ukusanyaji mapato.

Amewataka kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa kinara wa kuimarisha mahusiano ndani na nje ya nchi.


Katika kikao hicho Itunda ameipongeza ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Songwe, Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa kuendeleza mahusiano na ushirikiano hali inayochangia kuwa na amani na utulivu katika wilaya hiyo.

Dc Itunda amvaye tangu Rais Dkt Samia amteue kuwa mkuu wa wilaya Songwe imetulia na inason ga kimaendeleo huku.ushirikiano wa viongozi, wat endaji na chama ukiimarika siku hadi siku.


Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa