ENDELEENI KUSIMAMIA USALAMA NA KUJIPANGA NA UCHAGUZI MKUU, 2025.



Na Ibrahim Yassin Songwe

Maafisa na Wakaguzi wa jeshi la polisi Mkoa wa Songwe wametakiwa kujipanga kuhakikisha wana simamia usalama na kuendelea kujipanga na uch haguzi mkuu ujao ambao unatarajiwa kufanyika Octoba 25/mwaka 2025.

Hayo yamesemwa Februari 24, mwaka huu  na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga wakati alipofanya kikao kazi na Maafisa na Wakaguzi katika ukumbi wa Polisi uliyopo Vwawa Wilaya ya Mbozi.



Senga amesema ni bora maafisa hao wakaen delea kusimamia Askari katika himaya zao ili kutimiza jukumu mama la Jeshi la Polisi kwa kufuata sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili jamii iendelee kuwa salama.

"Endeleeni kutekeleza jukumu la kusimamia usalama wa raia na mali zao ikiwa ni pamoja na kujipanga na uchaguzi Mkuu, 2025 ili ufanyike kwa amani na usalama bila kujali itikadi ya chama chochote cha Siasa" alisema Kamanda Senga.



Kwa upande wao, Maafisa wamemshukuru Ka manda Senga na wameeleza kuwa wameji panga vyema kwa kuweka  mikakati endelevu ya kuima risha usalama kabla, wakati na baada ya Uchagu zi Mkuu ili uchaguzi ufanyike kwa utulivu na amani.

"Jeshi la polisi lina jukumu kubwa kuhakikisha linalibda raia n mali zao kwa.kusimamia na kuulin da utulivu uliopo hasa katika kipindi kijacho cha uchaguzi mkuu" amesema Senga.


Imekuwa ni kawaida kwa mkuu huyo wa polisi mkoani Songwe kutoa nasaa kwa jeshi la polisi akiwaasa vijana wake kuhakikisha wanaongeza weredi katika kutimiza majukumu yao.









Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa