DC ITUNDA AWATAKA VIJANA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUPAMBANA DHIDI YA UKATILI.


Na Ibrahimu yassin,Songwe

Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Solomon Itunda amewataka vijana hususani wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba kushiriki shughuli za maendeleo na kupambana dhidi ya wanaofanya ukatili katika jamii.

Dc Itunda mbali na kuwataka vijana hao kushiriki shughuri za maendeleo pia amawataka  kuimarisha ulinzi na kuwa kielelezo cha matendo mema katika jamii zao.

Mhe. Itunda alitoa wito jana  wakati akifunga mafunzo ya  Jeshi la Akiba 2024 katika Kata ya Gua  Wilayani Songwe.

Vijana 119 wamehitimu leo mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba katika Wilaya ya Songwe baada ya kupata mafunzo kwa miezi minne.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Itunda amewataka vijana hao kuzingatia mafunzo hayo ili yakawe na tija katika maisha yao na jamii.



Amesema kuwa vijana hao 119 wamepata stadi mbalimbali za kuwasaidia katika maisha yao ambao pia watasaidia kuimarisha usalama katika Kata ya Gua hali itakayochochea kukua kwa uchumi.

Mkuu huyo wa Wilaya amewasisitiza wahitimu hao kufanyia kazi kwa vitendo yale waliyofundishwa kwa miezi minne akisisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu imewekeza katika ulinzi hivyo wahitimu hao

 wakaendeleze mpango huo wa kuimarisha ulinzi na usalama katika ja
Awali akitoa taarifa ya mafunzo hayo, Mratibu wa mafunzo ambaye pia ni Mshauri wa Jeshi la Akib a, JF Cibaya amawapongeza vijana hao kwa kuhiti mu mafunzo salama.

Cibaya ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songwe pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Songwe kwa ushirikiano wao ambao umesaidia kufanikisha mafunzo hayo.



Comments

Popular posts from this blog

KAEGELE NA KAZUKAMWE WAIBUKA KIDEDEA KURA ZA MAONI CCM WILAYANI NKASI

DIWANI KATA YA KALA AFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIHARUSI

Mke wa Mchungaji wa kanisa la EAGT ajinyonga akihofia deni lake la fedha za kanisa